Mashindano ya vitivo Chuo Kikuu Mzumbe Kwa mwaka huu 2024 yamehitimishwa Mei 26, kuhusisha michezo mbalimbali na washindi kuondoka na zawadi ya Kombe, mipira na jezi.
kila mwaka Mzumbe imekuwa ikiiandaa mashindano hayo Kwa lengo la kukuza taaluma, vipaji, na mshikamano miongoni mwa wanafunzi.
Akihitimisha fainali za michezo hayo Amidi wa wanafunzi Bw. Alphonce Kauky amewapongeza washiriki wote na waandaaji wa mashindano hususani walimu na time zilizofika fainali kwa michezo yote na kutwaa ushindi.
“ Hakika mmefanya vyema nawapongeza sana kwa kujitoa na kuhakikisha tunapata time bora ili kutuwakilisha kwenye mashindano makubwa.” Alisema Bw. Kauky
Nae Mwalimu wa michezo Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Yohana Moises Magongo amesema michezo ni muhimu sana licha ya kujenga mwili pia hukuza kipaji, na kuboresha mapungufu aliyonayo mshiriki ili kujenga timu bora kuelekea mashindano makubwa yatakayofanyika mwezi wa 12 nchini Kenya.
“ Mashindano haya yanaongeza ari ya ushindani na kupata washiriki wazuri wa kutuwakilisha kwenye mashindano makubwa kama timu yetu ya mpira wa miguu na mpira wa pete hutung’arisha Kitaifa natoa rai kwa mabinti wenye vipaji wajitokeze kushiriki bila kusita.”
Katika hatua nyingine Amidi wa wanafunzi Bw. Kauky alikabidhi zawadi ya kombe na fedha taslim kiasi cha shilingi laki tatu (300,0000) kwa mshindi wa kwanza wa mpira wa miguu Skuli ya Sheria (Law) na shilingi laki mbili kwa mshindi wa pili wa mpira wa miguu kutoka kitivo cha Sayansi na Teknolojia (FST)
Pia kwa mshindi wa kwanza wanawake mpira wa miguu Mzumbe Queens kupata kiasi cha fedha laki mbili (200,000) wakifatiwa na mshindi wa pili Mzumbe Ladies waliojinyakulia kitita cha fedha laki moja na nusu(150,000)
Mpira wa kikapu kwa wanaume walioibuka Kidedea ni kutoka Skuli ya Usimamizi wa Utawala wa Umma (SOPAM) kwa kuondoka na kitita cha laki moja na nusu (150,0000) taslim na mshindi wa pili kutoka skuli ya biashara (SOB) kuondoka na kiasi cha shilingi laki moja (100,000) na zawadi nyingine zilitolewa kwa washiriki wote waliofanya vizuri. Mashindano haya huongeza ufanisi kwa washiriki na kuongeza nafasi za ajira kupitia kipaji walivyonavyo.
Post A Comment: