Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama tarehe 22.05.2024 imetoa elimu kinga juu ya madhara ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya kwa wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika migodoni mitatu ambayo ni _"Franonone Mining"_ wachimbaji 64, mgodi wa _"Iraq Mining"_ wachimbaji 50 na mgodi wa  _" Gems & Venture Mining"_ wachimbaji 64, katika Halmashauri ya Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro katika Mkoa wa Manyara. 

Aidha, DCEA Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana vyombo vya ulinzi na usalama  ilifanikiwa pia kufanya operesheni Mjini Mirerani na kufanikiwa kuwakamata watu sita waotuhumuwa kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya aina ya mirungi.

Wachimbaji wa madini ni miongoni mwa kundi muhimu. Hivyo, utoaji wa elimu kinga iliyotolewa kwa kundi hilo itasaidia katika kupunguza tatizo la dawa za kulevya katika eneo hilo.








Share To:

Post A Comment: