Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imezitembelea  Asasi za Kiraia sita zinazojihusisha na uelimishaji katika jamii juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya katika Mkoa wa Arusha. 

Lengo la Mamlaka kufanya ziara hiyo ni kuzitambua ofisi rasmi za Asasi hizo pamoja na kufahamu jinsi zinavyofanya kazi lakini pia kufahamu changamoto zinazowakabili wakati wa uteketezaji wa majukumu yao pamoja na kuwapatia vitendea kazi; Miongozo, Vitabu, Majarida na Vipeperushi.

Asasi hizo zilizotembelewa ni;  Youth and Community Rehabilitation (YCR), Drug Abuse and Recovering Organization (DARO), Care For All, BlueCross Society of Tanzania, Kimara Peer Educators na Youth Wings.

DCEA Kanda ya Kaskazini itaendelea kuzitembelea Asasi za Kiraia zinazojishughulisha na udhibiti na adhari za matumizi ya dawa za kulevya ili kuimarisha zaidi ushirikiano kiutendaji  pamoja na kuziibua Asasi nyingine mpya zenye malengo kama hayo ili kuiweka jamii ya Mikoa ya Kanda ya Kaskazini huru dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.








Share To:

Post A Comment: