Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndg. Mohammed Ali KAWAIDA (MCC) ameweka bayana kuwa Umoja wa Vijana wa CCM utaendelea kumlinda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Hali na Mali licha ya kuwa kuna watu wanapata homa kuona namna Rais Samia anavyotekeleza vyema Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 

Ndg. Kawaida ameyasema hayo wakati akizungumza na maelfu ya Vijana waliojitokeza kwenye Kongamano la Wasomi na Dkt Samia lililoandaliwa na Tawi la UVCCM Mabibo Hosteli Seneti Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika katika ukumbi wa Ubunge Plaza Ubungo Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Aprili, 2024.

"Nimefarijika sana leo kupata hii nafasi ya kubadilishana mawazo na ndugu zangu wa Chuo Kikuu upande wa Mabibo Hosteli niwaambie jambo moja wapo watu wanaweweseka na kupata homa zisizo na sababu wakiona namna ambavyo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anavyotekeleza vyema Ilani ya Uchaguzi ya CCM"

Lakini pia niwape salama kutoka kwa Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia anawasalimu sana na anaona namna Vijana mnavyoendelea kumuunga mkono kila siku.

"Rais wetu Mhe. Dkt Samia anaimani kubwa na Vijana na ndio maana Mwezi Machi, 2024 niliaminiwa na Chama cha Mapinduzi kwenda kusimamia Kampeni za Uchaguzi mdogo wa marudio wa Kata ya Kabwe katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa na tumefanikiwa kuirudisha Kata ya Kabwe kwenye mikono Salama ya CCM baada ya miaka 27 kuwa upinzani" amesema Ndg. Kawaida.

Aidha Ndg. Kawaida amempongeze Katibu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Ndg. Emanuel Martine kwa namna anavyofanya kazi kubwa sana, tangu nimteuwe hajaniangusha hata kidogo.

"Katika Uongozi wangu nataka kuwa daraja la kuwasogeza Vijana wenzangu natambua kuna Vijana wengi na wenye uwezo bado hawajapata nafasi."

Hata hivyo Ndg. Kawaida amewaonya wale wote wanaotumia mitandao yao ya Kijamii kumkashif na kumvunja moyo Rais wetu wasitumie vibaya uhuru wao wa kuzungumza, yupo mwanadada mmoja eti anajiita mtanzania, anaendelea kutumika kumchafua Rais wetu, UVCCM hatutamjibu mwendawazimu kwani UVCCM tumefundishwa kujibu hoja kwa hoja na bahati nzuri anahoja zake mbili Tozo na Umeme nani asiyejua faida za Tozo hapa" 

Mwisho Ndg. Kawaida amewapongez a Viongozi wa Tawi la UVCCM Mabibo Hosteli na Vijana wa Hamasa kwa kazi kubwa wanayoifanya pamoja na kusisitiza Vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.Share To:

Post A Comment: