IMG-20240413-WA0016
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwasa ikiwa ni mwanzo wa ziara ya kikazi ya bodi na menejimenti ya Mamlaka mkoani humo.. tarehe 13 Aprili, 2024.
IMG-20240413-WA0017
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo (hayupo pichani) akizungumzia jukumu la Udhibiti wa mbolea na namna Mamlaka imejipanga kuhamasisha usajili na matumizi sahihi ya mbolea ili kuongeza tija kwenye uzalishaji.
IMG-20240413-WA0018
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA,Dkt. Anthony Diallo (mwenye kofia) akizungumza katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa (hayupo pichani) akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo
IMG-20240413-WA0019
Meneja wa TFRA Kanda ya Ziwa Michael Sanga akizungumza jambo kuhusu utekelezaji wa mpango wa ruzuku katika mkoa wa Kagera katika kikao baina ya Bodi na Menejimenti ya Mamlaka na Mkuu wa Mkoa huo, Fatma Mwassa tarehe 13 Aprili, 2024.
IMG-20240413-WA0020
IMG-20240413-WA0021
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa akizungumza jambo mbele ya ujumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Anthony Diallo (mwenye kofia) walipofika ofisini hapo kwa ziara ya kikazi mkoani humo tarehe 13 April, 2024.

Na Mwandishi wetu ,  Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa ameipongeza Serikali kwa kuja na mfumo wa utoaji wa mbolea za ruzuku na kueleza zimeleta mwamko kwa wakulima na kuongeza uzalishaji.

"Serikali imekuja na mpango mzuri tunaufurahia kwani mbolea zinafika kwa walengwa hasa tofauti na mifumo iliyopita ambapo wachache walijinufaisha" Mwassa aliongeza.

Mkuu wa Mkoa, Mwassa ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Tanzania waliofika ofisini kwake kueleza lengo la ziara yao mkoani humo

Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo amesema, ziara hiyo imelenga kutoa hamasa kwa viongozi wa mikoa kuwasimamua kikamilifu maafisa ugani wa maeneo hayo kutoa taarifa sahihi za matumizi ya mbolea ili kusaidia kuwa na takwimu sahihi zitakazosaidia wakulima kufikishiwa pembejeo hiyo kwa wakati na kwa utoshelevu.

Aidha, Mwenyekiti Dkt. Diallo, ameuomba uongozi wa Mkoa wa Kagera kufuatilia matumizi ya vifaa vya kupimia afya ya udongo vilivyotolewa na serikali kwa maafisa Ugani ili kusaidia kutumia mbolea kulingana na mahitaji ya udongo.  

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent ameushukuru uongozi wa Mkoa kwa jitihada wanazochukua za kuhamasisha usajili wa wakulima na matumizi ya mbolea.

Amewahakikishia kuwa, Mamlaka itaendelea kusimamia ubora wa mbolea na kuhakikisha inamfikia mkulima karibu na shamba lake pamoja na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji wao.
Share To:

Post A Comment: