Mkuu wa Wilaya ya Ludewa- Mhe Victoria Mwanziva ameunga na Uongozi wa Chama na Serikali Wilayani Ludewa kuzungumza na vyombo vya Habari juu ya Miaka Mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan- Wilayani Ludewa.


Mheshimiwa Rais ameendelea kuonekana katika nyanja zote na Sekta zote Wilayani Ludewa ikiwemo;


HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA

Zaidi ya Bilioni 19 zinaendelea kutekeleza miradi ya Elimu, Afya, Maendeleo ya Jamii na Utawala Wilayani Ludewa 


SEKTA YA MAJI

Wilaya ya Ludewa inaendelea kutekeleza miradi saba (7) ya maji yenye gharama ya Tsh. 13,866,290,252.86

Kukamilika kwa miradi hii kunalenga kuongeza huduma ya maji kutoka asimia 74.3% hadi asilimia 79.7 eneo la vijijini na asimia 100% kwa wakazi wa mji wa Ludewa.


TARURA

Zaidi ya Bilioni 6 zimeelekezwa kutekeleza miradi ya Barabara Wilayani Ludewa- mfumo wa Barabara za TARURA.


TANROAD

Zaidi ya Bilioni 4 zimetolewa kwa ajili ya kuchonga Mlima Kimilembe- 

Na Barabara ya Zege ya Lusitu- Mawengi iliyogharimu zaidi ya Bilioni 179 inaendelea kutoa huduma na Barabara ya Zege ya Njombe-Lusitu inaendelea na ujenzi ili kuboresha miundombinu Wilayani Ludewa. 


KILIMO

Sekta Mama ya Wilaya ya Ludewa imeendelea kupata mkono wa Rais Samia kupitia Mbolea za Ruzuku, Pikipiki kwa Ma-Afisa Ugani wote Wilayani Ludewa, na utekelezaji wa mikakati makhususi kwa mazao ya Kimkakati Wilayani Ludewa.


VETA SHAURIMOYO

Wilaya ya Ludewa ina VETA ya Kimkoa- ambayo imegharimu zaidi ya Bilioni 6 na mradi huu utaenda kuleta mageuzi ya ki taaluma ya ufundi stadi Wilayani Ludewa na Mkoani Njombe.



MCHUCHUMA NA LIGANGA

Miradi ya Kitaifa ya Chuma na Makaa ya Mawe Wilayani Ludewa yameguswa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Bilioni 15 za fidia kwa wananchi wa maeneo ya Miradi ili kuendeleza shughuli za uchimbaji wa Madini haya kwa manufaa ya Taifa Letu.


Press Conference hii ilitoa nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Ndugu Sunday Deogratius kuelezea miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na Halmashauri kwa ushirikiano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Viongozi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa Ndugu Stanley Kolimba na Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa Ndugu Gervas Ndaki waliezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilayani Ludewa.


Uongozi mzima wa Wilaya ya Ludewa tumejidhatiti kwenye usimamizi wa Miradi, kwenye Utawala bora, kwenye kuwafikia wananchi mda wote ili kutimiza adhma ya maendeleo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan. 












Share To:

Post A Comment: