Mbunge Wa jimbo la Monduli Fredrick Lowassa Ameendelea na Ziara yake katika jimbo hilo kwa Lengo la kukagua Miradi ya Maendeleo , ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kusikiliza na kutatua Kero Mbalimbali za Wananchi katika Kata ya  Selela .

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa jengo jipya la Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Oltinga,  Wakati akisomewa taarifa ya jengo hilo Changamoto kubwa iliyoonekana ni uhitaji wa vitanda 104 Ambapo mbunge huyo alikubali kuichukua kama changamoto na kuahidi kufanyia kazi kwa wakati mfupi ili wanafunzi wapate pa kulala.


"Tumefika hapa tumetembea na tumezungumza na wanafunzi, Risala ikasomwa lakini kwa msisitizo zaidi ilikuwa ni changamoto la Bweni letu ambalo lilikuwa halina vitanda , kitu ambacho tunapaswa wote kujua Shule ya Oltinga ilianzishwa mwaka 2007, Shule ya Oltinga ni mmoja kati ya waasisi wa Shule za kata nchi nzima , Wakati mzee Lowassa anataka kuanzisha shule za kata nchi nzima alisema lazima kwanza aaanze na jimbo lake , kwa hiyo nilipofika pale nikasema pamoja na Changamoto zingine na mimi nataka niache Alama katika Shule hii ya Oltinga kwa kutoa vile vitanda 104 kulingana uhitaji wa Mwalimu mkuu katika taarifa yake" Amesema Fredrick


"Tumetoka hapo tukaenda kwenye tank kubwa hili hapa Ambalo linatoa maji lositeti, Ni Tank nimekaa na viongozi Nathani nimeambiwa Tank lile lilijengwa Mwaka 1951,  lilijengwa na wajerumani kwa Ajili ya kusaidia  mifugo kupata  maji Wakati ule , Mwaka 51 hata mzee Lowassa hakuzaliwa  hahhahahaha, lakini lazima tukubali technologia ya wenzetu pamoja na changamoto ndogondogo la Tank lile bado linaonekana lina uimamara sana , Nguvu za Wananchi ni kubwa kujenga Eneo la Mifugo kunywa Maji na Ripoti nimeona hongereni sana na kwa changamoto zilizobakia nimechukua ili kuzifanyia kazi" Amesema Fredrick

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja pia na Ujenzi wa Zahanati ya kitongoji cha Ranch kata ya Selela, Pamoja na Kushiriki Zoezi la ukabidhishwaji wa Kondoo na mbuzi 180 kwa wanawake  36 kutoka Shirika la PWC kitongoji cha SABURI -MAKUYUNI.


Wakati huo huo Amesisitiza Vijana kuchangamkia fursa za Mradi wa ujenz wa barabara kilomita 23 kutoka Mtowambu hadi SELELA , Inayotarajiwa kujengwa hivi karibu kwa lengo la kuwasaidia wakulima wa bonde hilo kusafirisha mazao yao.


Aidha kwa Upande wake Katibu wa Cha Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani humo Bi Rukia Mbasha Amesema lengo la Ziara hiyo Ni Mbunge kukagua ilani ya Chama, kuzungumza na Wananchi na kutatua kero zao.

"Yapo Maneno yalikuwa yanasambaa kwa Mh Mbunge hatumuoni hayo maneno yalikuwa yanakuja si kwa wema, yalikuwa yanakuja kwa ubaya kwamba mh mbunge katelekeza jimbo  sio mbunge tu hata mimi nisingeweza kufika, Baba yake ameugua miaka 3 Mzee lowassa Toka huyu Naingia Madarakani Mzee Lowassa anaumwa Mpaka Mwenyezi Mungu alipoamua kumpuzisha hivi hapa kweli tunaweza kumlaumu? Hapana, Leo hii baba yake hayupo tena kitandani tunamuona hatumuoni ? Tunamwona... Ndiyo huyo hapa tunaye na tutaendelea kutambana naye , kwa hiyo hizi hoja zinazoletwa watu hata kama wanataka nafasi ya mbunge wasubiri mda ukifika washindanishwe kwa hoja zao ,Sera zao Ahadi zao, lakini sio kwa sasa kuna mtu alikuwa hajui kwamba mzee Lowassa aliugua miaka 3? Na toka Fredrick achaguliwe si ni mwaka wake wa tatu? Alikuwa anatetea uhai wa baba yake  akitegemea mwenyezi Mungu atampa Tahafifu leo tuungane naye mzee wake lakini Imempendeza Mungu ,Wema wake na Fadhila tutamlipa kwa mtoto wake huyu hapa Fredrick " Amesema Rukia Mbasha


Share To:

Post A Comment: