Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amemshukuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kupendekeza Jina lake mbele ya Halmashauri kuu kuwa Katibu Mkuu UVCCM Taifa. 

"Nitumie fursa hii kumshukuru sana kutoka kwenye sakafu ya Moyo wangu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu; kwa Imani kubwa aliyonayo kwangu na hatimaye leo hii nasimama mbele yenu nikiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)".

"Vilevile; nawashukuru sana kwa Mapokezi haya ya Kipekee yamefana sana na yanaendelea kuthibitisha kuwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ndio Jumuiya nambari moja tegemezi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwamba Vijana tukipewa majukumu tunauwezo wa kuyasimamia kwa weledi mkubwa sana, nawashukuru sana".


Share To:

Post A Comment: