katibu wa siasa, uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa Joseph Ryata akiongea na walimu namna ya kutoa elimu ya udumavu na lishe bora ili kuondoa kabisa tatizo hilo ambalo limekuwa gumzo kwa miaka mingi mkoani Iringa 
katibu wa siasa, uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa Joseph Ryata akiteta jambo na viongozi wa walimu Makada wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa 
Baadhi ya walimu walimsikiliza katibu wa siasa, uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa Joseph Ryata Na Fredy Mgunda, Iringa.


CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimesema suala la mapambano dhidi ya udumavu na lishe bora sio jambo la kisiasa kila wananchi wa mkoa huo anatakiwa kutoa elimu hiyo.

Akizungumza na walimu katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,katibu wa siasa, uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa Joseph Ryata alisema kuwa mapambano dhidi ya udumavu na lishe bora halichagui chama ni jambo la kila mwananchi kwa mustakabali wa kuwa na kizazi bora hapo baadae.

Ryata aliwaomba walimu mkoa wa Iringa kuendelea kutoa elimu ya mlo kamili ili kuondoa kabisa udumavu katika mkoa huo ambao umekuwa na watoto wadumavu.

Alisema kuwa mlo kamili hauhitaji uwe tajiri ni mpangilio sahihi ya aina ya vyakula ambavyo vinaandaliwa na kuliwa majumbani ndio utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa udumavu.

Ryata alisema kuwa walimu wanamchango mkubwa wa kutoa elimu ya udumavu na lishe bora kwa watoto na wazazi kwa nyanja mbalimbali kulingana na taaluma waliyonayo.

Alimalizia kwa kusema kuwa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kinaendelea na mapambano dhidi ya udumavu na lishe bora kwa mstakabali wa kuwa na kizazi bora cha Taifa.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: