Kuelekea kwenye tamasha la utalii Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro baadhi ya wamiliki wa hotel kubwa wilayani hapo wamesema wamejipanga kupokea wageni watakaofika wilayani hapo Kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Nchi.

Akizungumzia mapema hii Meneja wa hotel ya Elephant Motel Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Juma Msami amesema wameamua kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Mkuu wa Wilaya hiyo kwakuendelea kuboresha huduma zao katika kutangaza utalii wa Same.

Msami amesema pamoja na tamasha hilo kuibua fursa za uwekezaji ndani ya Wilaya hiyo wao kama wadau wa maendeleo na watoa huduma wamekuwa mstari wa mbele kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii ndani ya Wilaya kwa wageni ambao wamekuwa wakifika ndani ya hotel hiyo.
“Sisi kama wadau na watoa huduma ya malazi, chakula na kumbi za mikutano tupo tayari kupokea ugeni utakaoingia wilayani Same kwenye tamasha hili na hata baada ya tamasha hili hii ni kuonyesha mshkamano kati yetu na serikali katika kutoa huduma sambamba na kutangaza vivutio vya utalii ndani ya Wilaya yetu kwani kwa kufanya hivyo tunaunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wetu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kutangaza utalii”.

“Lakini pia sisi Elephant Motel hapa Wilayani Same tumeendelea kutoa huduma hizo za kupokea wageni na kuwapa huduma bora kila siku hivyo basi hata kwenye tamasha hili tutaendelea kufanya hivyo kwaajili ya kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Mkuu wetu wa Wilaya ambaye yupo na nia ya dhati kabisa ya kubadiliaha Same ”
“Alisema Juma Msami”.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo ya Same Mkoani Kilimanjaro Kaslida Mgeni amesema kuelekea kwenye tamasha hilo wanatarajia kupokea wageni zaidi ya 2000 Kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Nchi watakaoshiriki kwenye tamasha hilo sambamba na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Mkomazi,msitu wa Chome na mlima kidenge.

Share To:

Post A Comment: