Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ameongoza harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Konde Usharika wa Sinai Jijini Mbeya ambapo amechangia zaidi ya shilingi milioni kumi na moja na jumla ya shilingi milioni hamsini zimepatikana katika harambee hiyo.

Pichani Naibu Waziri,Askofu Mstaafu Israel Mwakyolile na Edina Mwaigomole Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mbeya wakipokea maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi Grayson Nyamoga eneo la ujenzi.

Mwenyekiti wa ujenzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mbeya Edina Mwaigomole amesema jengo hilo litakapokamilika litagharimu jumla shilingi bilioni 2.2 na mpaka sasa zimetumika zaidi ya shilingi milioni mia tatu.

Share To:

Post A Comment: