Wananchi zaidi ya mia saba( 7), kutoka vijiji vitatu vinavyounda Kata ya Lemooti Wilayani Monduli ,wamefanya mkutano mkuu wa kata kwa lengo la kuomba serikali kuingilia kati hali ya sintofahamu juu ya ardhi yao waliyoitenga kwa ajili ya Malisho kuvamiwa na mtu aliyejitambulisha mwekezaji kudai  Eneo hilo ni la kwake.

Wananchi hao wamesema Hali hiyo imeendelea kuchukua sura mpya kufuatia uvamizi uliofanywa na Mr Brown aliyetanjwa kwa jina hilo kutoka kampuni ya MAASAI STEPs CONSERVATION kuwakamatakamata wananchi na mifugo akiwaamuru kutofanya shughuli yeyote katika eneo hilo kwani ni mali yake ,ilihali hakuna documents zozote zinazoonyeshwa umiliki wa eneo hilo.

Melelo mbiroi ,Thobiko Nalepo pamoja na Salome Emmanuel wameomba Serikali kuingilia kati sakata hilo kwanza kusitishwa kwa kamatakamata za wananchi kwani wanafilisiwa mifugo , na kukomalia kutoondoka wala kusimamisha malisho katika eneo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji ,Issaya Yasi mwenyekiti kijiji cha Lemoooti Amesema msimamo wao ni kukataaa mtu yeyote kuingia au kuchukua ardhi hiyo .

"Tunaomba tu serikali kuna migogoro ya ardhi inasababishwa na watu ambao yaani mtu anaibuka mahali bila kufanya research na kufanya Polisi shamba la kuwaumiza wananchi, juzi alikuja na askari wakawakamata watu 5 sasa hii ni taharuki ndani ya jamii haikubaliki na hatutakuwa tayari kwa mtu yeyote kuingia kwenye Ardhi hii" alisema Yasi 

Awali akitolea ufafanuzi wa mgogoro huo Diwani wa kata hiyo ya lemooti Mh Moines Leboi amesema katika hati 22 zilizopo Halmashauri ya Monduli moja wapo ni hatii hii ya kijiji cha oldonyo na liko ndani ya eneo hilo analodai  mwekezaji huyo ni eneo lake, na kusema lengo la mwekezaji huyo ni kuja kuchimba bwawa eneo hilo ili kuwafuga wanyama, ilihali wanyama wamekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo.

Herieth Rugalabamu afisa ardhi monduli, Amesema katibu mkuu alishaelekeza Wilaya ya Simanjiro kwa kushirikiana na Mr Brown kuweza kulioondoa Eneo la Monduli lililozidi katika hati aliyopewa simanjiro lakini cha kushangaza hadi sasa , mtu huyo hakutekeleza Maagizo hayo.

Malalalmiko hayo yalimuibua Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ambaye Amewataka wananchi hao kulinda ardhi yao kwani kama halmashauri hawamtambui mwekezaji huyo na kusema tayari Katibu mkuu wizara ya ardhi ana taarifa hiyo , na alishaandikiwa barua mwekezaji huyo kuachia eneo la Ardhi ya Monduli kwani Eneo alilopewa ni kutoka simanjiro lakini yeye aliingia hadi eneo la Monduli na tayari alishaandikiwa barua kuachia mara moja eneo hilo.

" Naomba niwaulize ardhi hii ni ya nani....ya kwetu,sasa kwanini mnahangaika? Huyu bwana Brown kama alivyoeleza Afisa ardhi Monduli jamaa huyu alipewa eneo simanjiro yeye kachanganya na kujipimia hadi ardhi ya monduli niwahakikishie eneo hili ni la Monduli, na nimuelekeze mr brown kuachia eneo hilo wakati tunamalizia makubaliano na maagizo ya katibu mkuu Kamishna wa Ardhi na asimamishe mara moja kamatakamata za wananchi , haiwezekani mtu unakamata mifugo ya wananchi halafu unaenda kufanya kitoweo cha wafanyakazi wako haiwezekani , wana lemooti ardhi hii ni ya kwenu , tumieni kwa matumizi mliokubaliana na haitatokea mtu kuwasumbua tena " alisema Issack kadogo.

"Pamoja na Malalamiko hayo Tusimsahau pia kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Fedha za maendeleo anazoendelea kuelekeza katika halmashauri yetu na kata ya lemooti ni miongoni mwa wanufaika, juzi kwenye hotuba yake alisena viongozi tokeni maofisini nendeni kwa wananchi kafanyeni kazi nami leo naanza na hili leo 3.1.2024 naanza na hili la kusikiliza kero zenu hapa na msimamo wangu kama ninyi mlivyosimamia hilo ni kwamba Eneo hili ni mali ya Monduli ,ni mali ya Lemooti fullstop , Katibu mkuu Ardhi analijua hili kaeni kwa Amaani hakuna mtu wa kuwabughudhi."alisema Issack .

Share To:

Post A Comment: