NA DENIS CHAMBI,  TANGA.

MKUU wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amatoa onyo kali kwa wanajamii hususani wanaume ambao wamekuwa wakijihusisha na mapenzi na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  huku wakiwaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa huo  kusimamia  na kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote ambaye atabainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Kindamba amatoa kauli hiyo leo january 8 mara baada ya kutembelea shule za msingi Bombo na sekondari Old Tanga kukagua hali ya kuripoti kwa wanafunzi  kwa mwaka mpya wa masomo 2024 ambapo pia amatoa onyo kwa wazazi na walezi ambao wamekuwa wakimaliza kesi kifamiliya na wahusika mara baada ya watoto wao kupata ujawazito.

"Nitoe tahadhari kwa baadhi ya wanajamii wasiokuwa na mwenendo mwema wanaitwa mafataki wanaotembea na  wanafunzi wakati wangu kama mkuu wa  mkoa wa Tanga  sitavumilia , sitastahamili walasitakuwa na simile na mtu  yeyote anayeharibu maisha ya mwanafunzi ,  ukitaka kufanya hivyo chukua umri wako jumlisha na miaka 30 ya gerezani uone utatoka ukiwa na umri gani" alisema Kindamba

"Niwatake wakuu wa wilaya kote walipo kusimamia watoto hawa wale wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi na watoto wa shule wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi yetu,  nimeanza kupata kesi kutoka kwa baadhi ya  wazazi kesi zikishaenda mahakamani baadaye wanawaficha watoto au wanakaa kikao kifamiliya  mtu yeyote atakayecheza na watoto wa shule ajue anacheza na watoto wa serikali" alisisitiza.

Aidha amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto  shule  baadala ya kubaki nao nyumbani  huku akisisitiza michango yote itakayokuwa wakichangishwa wazazi na walezi kwaajili ya wanafunzi lazima iwe imepata kibali kutoka kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa.

"Mheshimiwa Rais  ameshatoa fedha kwaajili ya watoto wote wawe wanasoma bila ya ada kwahiyo kusiwe na kisingizio cha wazazi kutoleta wanafunzi kwenye mashule sitaki kusikia michango ambayo haina kichwa wala miguu michango yote inayochangwa kwenye mashule ni lazima iwe na kibali kutoka kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa"

Kindamba amezipongeza shule za Msingi Bombo na sekondari Old Tanga kwa kuvuka lengo la kusajili wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2024 ambapo shule ya msingi Bombo ilitarajia kusajili wanafunzi 70 na imefika 71 huku Old Tanga ambayo ilitarajia kusajili wanafunzi 114 ambapo amesema wataendelea kutembelea na kukagua kuona wanafunzi ambao wamesharipoti .

Akitoa taarifa kuhusu wanafunzi ambao wamesharipoti mkuu wa shule ya Old Tanga Juma Mgunya amesema kuwa shule hiyo awali ilipangiwa kupokea wanafunzi 114 lakini ikaongezewa wengine 86 wa uhamisho hivyo kufikisha jumala ya wanafunzi 200 ambao wote watapata viti pamoja na madawati pindi wawapo darasani.

"Shule ya Old Tanga ilipangiwa kupokea wanafunzi 114 lakini nmeongezewa wanafunzi wengine wa uhamisho na sasa jumla tuna wanafunzi 200 na mpaka sasa  ambao wameshafika ni wanafunzi 109  kati ya wanafunzi 200 ambao nimepangiwa ,  wanafunzi wote walipangiwa shule ya Old Tanga watakuwa na viti pamoja na meza   ambazo zitatosha kutokana na wanafunzi wa kidato cha nne ambao walimaliza mwaka jana" alisema Mwalimu Mgunya.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Bombo Denis Mushi amesema kuwa shule hiyo ilitarajia kusajili wanafuzi 70  ambao wamefanikiwa na kufika 71 kwa upande wa darasa la  awali  huku darasa la kwanza  wakitarajia wanafunzi 120 mpaka sasa wamesajili wanafuzi 121 na hivyo kufikisha wanafuzi 1002 kwa shule nzima kwa mwaka huu wa masomo.

"Shule ya Msingi Bombo iliweka maoteo ya kusajili wanafunzi 70 kwa darasa la awali na mpaka hivi sasa tumesajili wanafunzi 71 na  kwa darasa la kwanza tuliweka malengo ya kusajili wanafunzi 120 na mpaka leo tumeshasajoli wanafunzi 121 na hivyo kufikia asilimia 100 ya malengo  kwa darasa laawali na la kwanza hivyo baafa ya usajili huu shule itakuwa na jumla ya wanafunzi 1002 wavulana 492 na wasichana 510" alisema Mwalimu Denis

Alisema  shule ya msingi Bombo ilipokea kiasi cha shilingi Milion 81, 300,  000 kwaajili ya kutekeleza mradi wa BOOST kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo ambapo ujenzi huo umekamilika na tayari madarasa yanatumika na hivyo kuondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi katik vyumba vya madarasa.

"Tulipata  mradi wa BOOST ambao ulitekelezwa hapa shuleni kwa mwaka 2023 ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na matundu ya matatu ya vyoo ujenzi huu ulighalimu kiasi cha fedha Milion 81, 300, 000  kutoka serikali kuu na ujenzi huu umekamilika kwa aailimia 100 tunaishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali ya mkoa wa Tanga kwani mradi wa BOOST uliotekelezwa umepunguza msongamano mkubwa wa wanagunzi katika vyumba vya madarasa" aliongeza

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kinamba akiwa amekaa kwenye dawati na wanafunzi wa shule ya msingi Bombo mara baada ya kutembelea shuleni hapo leo january 8,2024.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akiwa amekaa na wanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi Bombo iliyopo jijini hapa mara baada ya kutembelea shuleni hapo kukagua kuwasili kwa wanafunzi hao kwa mwaka mpya wa masomo 2024.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akifundisha baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Bombo alipotembelea shuleni hapo kukagua wanafunzi walisajiliwa tayari kwa kuanza masomo kwa mwaka 2024.


Share To:

Post A Comment: