Na John Walter-Manyara
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amekabidhi Misaada Mbalimbali kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera ,Bunge na Uratibu ) Mhe Jenista Mhagama walioathirika na Mafuriko wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Chatanda amesema msiba huo mzito umeshtua Taifa na kwamba Umoja wa wameamua kujikusanya kwa Umoja wao kupeleka Misaada hiyo ambayo itasaidia wahanga.
"Sisi tulikuwa Rufiji kwenye Tamasha la Kumuenzi Bibititi Mohamed, lakini tukapata taaharifa hii na baadae tukaona kwenye Vyombo mbalimbali vya Habari tukasema kweli hali ni mbaya ndivyo tukaketi na kamati yangu ya Utekelezaji tukaamua tuje na hiki kidogo kwa ajili ya kurejesha tabasamu kwa watu ambao wamepata shida hii "Amesema Chatanda.
Post A Comment: