Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Shukrani kwa Mlipakodi iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Jijini Tanga


 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Shukrani kwa Mlipakodi iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Jijini Tanga










Na Oscar Assenga,TANGA



MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Tanga imefanikiwa kukamata mizigo yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.59 Kufuatia doria mbali mbali za kiforodha ziliyofanywa na mamlaka hiyo.

Doria hizo ni moja ya mikakati kabambe ya mamlaka hiyo kuhakikisha wafanyabiashara wanapita njia halali na kulipa kodi ya Serikali.

Akizungumza wakati wa wiki ya shukrani kwa Mlipakodi Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Thomas Masese alisema kwamba miongoni mwa bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na vitenge maroba 180 ambayo yalipigwa mnada na kiasi cha Milioni 328.2 kilikusanywa.

Masese alisema kwamba kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wamekusanya kiasi cha shilingi Bilioni 214.39 lakini pia kuna changamoto mbali mbali ikiwemo wafanyabiashara kukwepa kodi.

Awali akizungumza katika maadhimishio ya wiki hiyo Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu aliipongeza mamlaka hiyo kwa kuweka utaratibu huo wa siku ya shukrani kwa mlipa kodi kurejesha shukrani kwao.

Alisema walipa kodi ni muhimu kwa Taifa huku akiipongeza mamlaka hiyo kwa ukusanyaji wa kiwango hicho cha kodi kwani kila mwaka wamekuwa na ongezeko la mapato.

“Nikupongeze Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga kazi isingeweza kufanikiwa bila kusimamia vizuri wafanyakazi ambao nao wamefanya kazi kwa waledi kuhakikisha kodi inakusanywa “Alisema

Mwakilishi huyo wa Mkuu wa Mkoa aliwahamasisha waongeze kasi ya kuvuka lengo la kila mwaka ikiwemo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi .

“Kwa lengo la kuhakikisha mnaendelea na ongezeko la ukusanyaji wa mapato lakini pia kusanyeji kodi kwa waledi,uwajibikaji uadilifu na kujenga mahusiano ya karibu ya mazuri na walipa kodi”Alisema

Hata hivyo alisema nchi nyingi duniani zinategemeaa kodi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake hivyo ni muhimu watanzania watambue kwamba ulipaji wa kodi una manufaa makubwa .

Maadhimisho hayo ya siku y,a mlipa kodi yamekwenda sambamba na utoaji wa vyeti vya kuwatambua wafanyabiashara ambao wanajituma kulipa kodi.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: