Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amefanya Mkutano wa Hadhara na wananchi wa kijiji cha Buger kata ya wilaya ya Karatu kutafuta suluhu ya mpaka kati ya kijiji cha Buger na hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.

Katika Mkutano huo, wananchi wa kijiji cha Buger wanaiomba Serikali kuridhia mpaka wa maridhiano wa awali, uliofanywa baina ya tume ya baraza la mawaziri na wananchi hao ili kuwawezesha kuendelea kuishi hapo pasipo na mgogoro wowote.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano huo, wananchi hao wameeleza kuwa awali Mamlaka ya Hifadhi za Taifa iliweka mipaka ya Mikaratusi na kupakwa rangi nyekundu kama ishara ya mpaka kwa makubaliano na baadae kuboreshwa kwa kuwekwa nguzo kubwa hakukuwa na mgorogoro,ndipo baadae ikawekwa mipaka mingine ambayo wanasema haikushirikisha wananchi ndipo mgogoro huo ulipozuka.
“Sisi tuniomba Serikali kupitia wewe Mkuu wa Mkoa itukubalie kurudisha mpaka wa awali tuliyokubalina kwasababu huu mpaka ulioleta mgogoro umesababisha na makazi ya baadhi ya wananchi kubaki kwenye hifadhi”. Amesema Samson bayo, Mkazi wa Buger.

Sambamba na hayo, wananchi hao wameishukuru sana Serikali kwa kuendelea kuwajali pamoja na kumshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa kutumia hekima kubwa na busara katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwani wanaamini utaisha salama bila kuleta mgogangano wowote.
Tunatambua sana umuhimu wa hifadhi hii hususani katika maeneo yatu haya, hivyo tunaishukuru sana Serikali kwa kuwa inatusikiliza na kutafuta namna bora ya kumaliza mgogoro huu kwa njia ya makubaliano”. Amesema Emmanuel Matay, Mkazi wa Kijiji hicho.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella amewaeleza wananchi hao nia njema ya Serikali ya kuweka mipaka hiyo kwa kukwepa makazi ya watu waliokwisha kuvamia eneo la hifadhi na kuendelea na shughuli zao za maendeleo.
Hata hivyo, Mhe. Mongella baada ya kuwasiliza wananchi hao, ametoa siku 10 kwa wahifadhi wa hifadhi hiyo kushirikiana na wajumbe watatu walioteuliwa kwenye Mkutano huo kuwakilisha wananchi kufanya tathimini ya eneno hilo na kubaini eneo la mpaka unapopaswa kuwekwa kulingana na ramani ya hifadhi hiyo kisha kuandaa taarifa na kuiwasilisha kwa Mkuu huyo wa Mkoa kwaajili ya kumaliza mgogoro huo kwa kuweka mipaka ya kudumu.
Awali, kutokana na mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka nane, umesababisha kusimama kwa shughuli za uwekezaji wa hifadhi hiyo na kuingizia Serikali mapato kupitia mapato yatokanayo na utalii.


Share To:

Post A Comment: