ARUSHA: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya amewataka wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Arusha pamoja na wanachama wa chama hicho kurejesha sura mpya, heshima, nidhamu na utaratibu ndani ya chama hicho.

Sabaya amesema hayo wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha ambapo ameweka mkazo kwenye swala zima la nidhamu na kujali muda wa vikao.

“Tunaomba ugonjwa huo wa muda uondoke naomba sana, niliahidi siku Ile kwamba tutakwenda kwa kukimbia kidogo ili tufufue uhai wa chama mpaka kule chini, tuonekane kwamba sio wale bali ni watu wengine wapya ambao tunajiandaa kwa ajili ya uchaguzi tukiwa mchakamchaka” alisema

Amesema upo ugonjwa kwa baadhi ya wajumbe kuja kwenye vikao aonekane na kuandika jina huku wakiwa wamekuja muda wanaojiskia wao na kutoka kabla ya kikao kuisha, mazoea hayo ameomba yaondoke

“Sasa umekuja kufanya nini?, sisi tumechaguliwa, unaaminika,watu wa chama na watu wa serikali wanakuwa wewe ndio mwakilishi wao halafu unakuja unajionyesha halafu unaondoka, mazoea hayo naomba yaondoke”alisema

Amesema kuwa kama umepewa dhamana basi heshimu dhamana hiyo, kama wewe ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Arusha, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Arusha, simama kwa nafasi yako na uonekane unashiriki na utoe maoni na ushiriki kikamilifu.

Share To:

Post A Comment: