Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB bw.AbdulMajid Nsekela akizungumza na Washiriki wa Michuano ya CRDB Super Cup ambao hawapo pichani.

 Msimu wa tatu wa mashindano ya CRDB SUPA Cup yaliyoandaliwa na Benki hiyo yamemalizika mkoani Arusha Katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Timu ya Ulipo Tupo FC kutoka Kanda ya Ziwa imefanikiwa kutwaa Ubingwa baada ya kuifunga SDK Football Club ya Kanda ya Mashariki (Dar-es-salaam) magoli 2-1.


Mashindano hayo yamelenga kudumisha umoja miongoni mwa wafanyakazi wa Benki hiyo nchini kupitia Michezo mbali mbali ambapo pia ni fursa ya kuimarisha afya zao kupitia mazoezi na kuongeza ufanisi kazini.

Bi.Crescensia Grace Kajiru kutoka Idara ya Rasilimali Watu ya taasisi hiyo alisema kulikuwa na timu 12 za mpira wa miguu na timu nane za mpira wa Pete ambapo katika michuano ya Kombe la CRDB Bank Supa iliyoanza tangu Agosti 20,2023 na yalizinduliwa jijini Dar-Es-salaam na kufikia kilele Desemba 2023 Jijini Arusha.

"Lengo ni kuwakutanisha Wafanyakazi wetu pamoja na kuimarisha afya kwani mara nyingi wanakuwa wamekaa wakihudumia wateja pia kupitia michezo hii inawalazimu kuwa na mazoezi, na kama mnavyofahamu benki yetu ni kubwa sana hivyo wafanyakazi wanawasiliana Kwa simu tu hapa tumekutana wote kupitia Michezo hii ni faida nyingine ya kukuza mahusiano na kuongeza ufanisi katika kazi zetu"Alisisitiza bi.Kajiru

Bi.Kajiru alisema kuwa kupitia Timu hizo 12 zilizoanza makundi hatua ya robo fainali zilishiriki Timu 8 Kwa upande wa Moira wa miguu wanaume,Timu nne nusu fainali na timu mbili ambalo Ulipo Tupo imeibuka mshindi na kujinyakulia Shilingi Milioni 13 taslimu.

Timu bingwa katika soka ilijinyakulia kombe medali ya dhahabu na kitita cha Milioni 13, mshindib wa pili akipata milioni 9/- kikombe, huku washindi wa tatu akipata milioni 6.

Aidha katika mpira wa Pete Kwa upande wa wanawake mshindi alipata milioni 13, mshindi wa pili milioni 8 na mshindi wa tatu Milioni 4 ambapo kiasi kadhaa Cha Fedha kuongezwa na Viongozi ambao ni wakuu wa idada mmbali mbali ndani ya benki hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Kwa washindi mara baada ya kumalizika mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Arusha bw.Felician Mtehengerwa ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema alizipongeza Timu zote Kwa kushiriki michuano hiyo na kuwataka kuongeza bidii mwakani Kwa ambao hawakushinda mashindano hayo.

"Benki ya CRDB imekuwa kinara mwenye mambo mengi na hapa tunaona kwenye michezo pia mmefanya vizuri hamna jambo dogo kabisa na niwaombe uongozi mmeona namna ambavyo vijana wametoka jasho hapa wote wamecheza Mchezo mzuri sana na niombee muendelee kulea hii Timu ikiwezekana upande ligi Kuu."Alisema Mtahengerwa

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB bw.AbdulMajid Nsekela alisema kuwa Timu zote zimeonyesha kiwango kizuri na aliyeshinda amestahili na kuahidi kuwa benki hiyo itaendelea kuboresha Mashindano hayo Kila mwaka,na kuwataka wachezaji kuongeza viwango zaidi.

kwa upande wa Netiboli Ulipo Tupo Queens kutoka Mwanza k walifanikiwa kuifunga timu ya CRDB ya Kanda ya Kati ijulikanayo kwa jina la 'Popote Ina tiki kutoka Dodoma kwa mabao 45 – 23 katika mchezo wa fainali zilizofanyika uwanja huo huo.

Baadhi ya wachezaji wa Ulipo Tupo Kanda ya Ziwa ambayo imetwaa Ubingwa wa michuono hiyo.

Share To:

Post A Comment: