Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) yaungana na waandishi wa habari jijini Arusha kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya
Akifungua kikao hicho msaidizi wa katibu tawala na utumishi wa rasilimali watu David Lyamongi ,jijini Arusha katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Arusha aliwaasa waandishi wa habari kutoa ushirikiano pamoja na kuelemisha jamii ,kutoa taarifa mbali mbali za wauzaji na watumia wa dawa za kulevya
Kwa upande wake msimamizi wa elimu ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Mkoa wa Arusha Shabani Miraji alitoa elimu kwa waandishi wa habari juu ya madhara pamoja mikakati waliyoiweka ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kitaifa , kikanda na kimataifa
Aidha aliongeza kuwa dawa za kulevya ni hatari katika jamii kwani zinamadhara ya kifya,kijamii,kiuchumi, na kimazingira ya hivyo wote tunapaswa kuyatokomeza.
Post A Comment: