Katika picha ni muonekano wa majengo ya Kituo hicho cha Afya kilichopo wilayani Ngorongoro
 Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella akimjulia hali moja ya mgonjwa alipotembelea katika kituo hicho cha Afya.


 Wananchi wa Kata ya Sale wilaya ya Ngorongoro wameishukuru serikali kwa upanuzi wa Kituo cha Afya cha Waso,ambapo ni takribani kilometa 49kutoka makao makuu ya wilaya eneo hilo zaidi ya wakazi takribani 6,579,ambao watapatiwa huduma za kiafya kutoka katika kituo hicho.


Akizungumza mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella alipokuwa katika ziara ya kikazi pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na serikali alisema kwa kipindi kirefu katika eneo hilo hawakuwahi kuwa na kituo cha afya, zaidi walikuwa na zahanati ndogo ya kijiji, ambayo ilitoa huduma lakini kutokana na ongezeko la idadi ya watu ilifikia kuelemewa na kushindwa kumudu kuwafikia wananchi wote.

Alisema kuwa Wananchi wa Sale hususani wanawake, walilazimika kwenda eneo la Waso kupata huduma za kujifungua jambo ambalo liliwagharimu muda na fedha na kusababisha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua kutokana na ucheleweshwaji wa kupata huduma stahiki.

Bi. Hosiana ni mama wa watoto watatu ambaye ni mgonjwa wa kwanza kujifunga katoa wodi ya wazazi, anasema watoto wake wawili alilazimika kufunga safari mpaka Waso umbali wa zaidi ya Km 50 kutoka eneo hilo ili kwenda kujifungua ambapo ilimpa gharama kubwa za fedha na muda sambamba na kuwapo na kinamama waliopoteza maisha kwa kuchelewa kupata huduma za kujifungua.

"Kuna wajawazito walipoteza maisha kwa kukosa huduma ya kuongezewa damu, ilikuwa mpaka uenda Waso, kama huna pesa, ilikuwa ni tatizo kwa familia nyingi, wakati mwingine tulilazimika kuchangishana ili mtu akapate huduma, kwa sasa hakuna tena hayo maisha"alisema

Wananchi hao wameweza kutoa shukrani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia kwa kuwajengea kituo cha afya, kwani kitawasaidia kuwapunguzia mwendo na gharama za kufuata huduma mbali, sambamba na kupunguza vifo visivyo vya lazima kwa wanawake na watoto wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Jenifa Ismael Legina licha ya kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kujenga kituo cha afya Sale, amethibitisha kituo hicho kutaondoa vifo visivyo vya lazima hasa kwa wanawake wakati wa kujifungua kwa kuwa, kituo hicho kinatoa huduma bora kikiwa na madaktari wazuri wenye moyo wa kuwahudumia

"Sisi wanawake wa Sale tunamshukuru Rais wetu, mama Samia ametujali wakinamama, tuna uhakika wa afya za familia zetu, watoto wawili nilijifungulia Wasao, ukiwa huna pesa unaweza kupoteza maisha" Amesema Hosiana

Ikumbukwe kuwa serikali ilitoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa zahanati na kuwa kituo cha afya na tayari imeshatoa milioni 38.5 kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.
Share To:

Post A Comment: