Picha za Ndege zilizounganishwa na kutengenezwa katika kiwanda cha Airplane Africa Limeted kilichopo Mazimbu Mkoani Morogoro, kiwanda hicho kinamilikiwa na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech.
Baadhi ya wanafunzi wa kiwanda cha ndege cha Airplane Africa Limeted akiendelea na kazi ya kuuunganisha bawa la ndege ,kiwanda hicho kinamilikiwa na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech.
Katibu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara (Kulia)akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Maswala ya anga Endruu Magombana (kushoto) wakiwa ndani ya moja ya ndege zilizotengenezwa na kuunganishwa katika kiwanda cha Airplane Africa limited kilichopo Mazimbu Morogoro.
Katibu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akishuka katika moja ya ndege zinazotengenezwa na kuunganisha na kampuni ya kiwanda cha cha Airplane Africa limited kilichopo Mazimbu Morogoro.
Picha za Ndege zilizounganishwa na kutengenezwa katika kiwanda cha Airplane Africa Limeted kilichopo Mazimbu Mkoani Morogoro, kiwanda hicho kinamilikiwa na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech.

Na Mwandishi wetu - Morogoro 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyrara amesema kuwa wizara yake inategema kukutana na Wizara ya Fedha ili kuweka utaratibu wa kusidia sekta ya Anga hasa kwa kampuni zinazounganisha na kutengeneza ndege hapa nchini.

Kahyrara amesema hayo baada ya kutembelea Kampuni ya Airplane Africa Limited iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro inayomilikiwa na wawekezaji kutoka jamhuri ya Czech ambayo inafanya kazi ya kuunganisha na kutengeneza ndege za kubeba abiria wawili mpaka wanne.

“Uwekezaji huu ni mkubwa na hivyo nitawasiliana na wizara ya fedha ili tuone naona ya kuwekea mazingira mazuri wawekezaji hawa” alisema Kahyarara

Kahyrara ameongezea kuwa mafundi wanofanyakazi katika kiwanda hicho engi wao wamesoma chuo cha usafirishaji (NIT)hivyo ni muhimu kwa kiwanda hicho kwani kitasaidia kutoa uzowefu kwa wanafunzi wa kutoka vyuo vya Vikuu, , vyuo vya kati na Vyuo vya Ufundi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho Mhandisi Igor Stratl amesema kuwa wamevutiwa kuwekeza Tanznia kwasababu ni nchi yenye Usalama, Utulivu na Amani hivyo imewarahisishia kufanya kazi zao muda wote .


Lilian Petrol ni moja wa mafundi katika chuo hicho amesema kuwa ufundi wa kutengeneza ndege ameipata katika chuo cha usafirishaji cha (NIT)hivyo imemasadia kufanya kazi katika kiwanda hicho hivyo anaiyomba serikali kuendelea kuongeza vivutio zaidi ili wawekezaji zaidi waweze kuja na vijana kuendelea kupata ajira.

Kiwanda hicho kilchoanza mwaka 2021 mpaka sasa kimeunganisha na kutengeza ndege zaidi ya tatu na ndege hizo zinaweza kuuzwa katika nchi mbalimbali .
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: