Ashrack Miraji Same kilimanjaro

Mbunge wa Same Magharibi DKT David Mathayo amesema michezo inawajenga vijana kuwa na mahusiano mazuri Katika nyanja mbali mbali na kuweza kutimiza Ndoto zao pia kuachana na vitendo viovu kama ukabaji na kutumia madawa ya kulevya, bangi na Mirungi 

Hayo ameyasema leo wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wetu Katika kuelekea uzinduzi wa  Mathayo Cup tarehe 26 November Katika jimbo la Same Magharibi Mkoani kilimanjaro ambazo Timu 56 zitakwenda kushiriki mashindo hayo

Dhamila Yangu kwa vijana ni kubwa Mno ni kutaka kuona wanafika mbali na kutimiza Ndoto zao hivyo ntakuwa nao bega kwa bega Katika kuleta Maendeleo chanja kwenye jimbo letu la Same Magharibi kuakikisha na kuza vipaji vyao Alisema Dkt David Mathayo Mbuge wa jimbo la Same Magharibi

Mhe Dkt Mathayo amesema pia Mathayo Cup hii ni jitiada za kumuunga Mkono Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samiha Suluhu Katika sekta za Michezo tumeona Rais akifatilia Michezo tofauti kwa ukaribu Sana pia na kuzipa Timu zetu hamasa Katika mashindano ya kimataifa na Mimi kama muhakilishi wake Katika jimbo la Same Magharibi ntaakikisha vijana wa Same Magharibi wananufaika Katika Michezo na Shughuli Mbalimbali za kiuchumi

Pia nisiwe mchoyo wa fadhira na niseme ukweli wa dhati kwa Mhe Rais Dkt Samiha Suluhu Hassani amenifanyia makubwa Katika jimbo langu amenijengea vituo vya Afya Barabara shule namshukur sana kwa Mchango wake mkubwa hasa kwa Wananchi Wang wa jimbo la Same Magharibi hivyo niwaombe wananchi wa jimbo langu kuendelea kumuunga Mkono Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa Kazi kubwa anayoifanya Katika kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu na Taifa.




 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: