Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Wilson Mahera amewataka maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kutumia mafunzo wanayoyapata kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. 

Dkt. Mahera ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Maafisa TEHAMA wa Mkoa wa Dodoma kuhusu mfumo huo mapema jana tarehe 13.11.2023 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

Amesema ‘Maafisa TEHAMA wanapaswa kutumia ujuzi watakaopata kupitia mafunzo haya na  kwenda kuwafundisha watumishi wa ngazi za kutolea huduma za Afya kwenye vituo vya kutolea huduma kwa ngazi za Halmashauri.

“Nyie sasa ni TOT (Trainer of Trainees) tujenge uwezo kwa watumiaji wa GOTHOMIS na watumishi wengine katika ngazi zote kwenye vituo vya kutolea huduma pamoja na usimamizi wa karibu na matengenezo ya mfumo huu “ amesema Dkt. Mahera.

GOTHoMIS ni mfumo unaosimaia shughuli za Hospitali Tanzania na unatumika kwenye Vituo vya kutolea huduma nchini

Mafunzo ya mfumo huu yametolewa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na KOICA na PMC.



Share To:

Post A Comment: