Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa baadhi ya watendaji sekta ya ardhi wasiokuwa wema wamekuwa wakiwahonga baadhi ya viongozi kwa kuwapa viwanja kama kinga yao mara wanapokutwa na makosa ili hali viongozi hao wanakuwa hawana taarifa kama watendaji hao wana nia ovu.

Waziri Silaa amesema hayo mara baada ya kufika eneo la eneo lenye mgogoro linalomilikiwa na kanisa la Morovian kiwanja namba 1,2 na 3 Block T mtaa wa Itega Jijini Dodoma.

Waziri Silaa amesema aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru anahusika kwa kiasi kikubwa na dhuluma za viwanja Jijini Dodoma makosa aliyoyatenda kwa kutumia cheo chake kama Mkurugenzi wa Jijiji au yeye binafsi kama Mafuru kudhulumu haki za wengine.

‘’Kuna wakati Wakurugenzi wa Mamlaka za upangaji na watendaji Wizarani ambao wamekuwa wakipima viwanja kwa watu wenye nguvu na kuacha kumpimia ardhi ambaye hana nguvu, katika uongozi wangu kama Waziri mwenye dhamana nitaweka mstari uliyonyooka na stashiriki katika dhammbi kama hii.’’ Alisema Waziri Silaa.

Kwa upande mwingine mchungaji wa kanisa la morovian  amemshukuru Waziri Slaa na Serikali kwa ujumla kwa kufika eneo la tukio na kutatua mgogoro uliowakabili kwa muda mrefu kwani wameteseka kwa kipindi kirefu na mgogoro huo bila kuwa na mafanikio.

Share To:

Post A Comment: