Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Manyara Mwl.Mugisha Galibona Kwa niabaya Katibu tawala Mkoani hapa  ametoa wito Kwa Viongozi wa kata ya Luxmanda Halmashauri ya Wilaya ya Babati Kuwa na ukaribu na watoto wao wanaoishi nje na Nyumbani yaani (Geto) kwani ni chanzo kikubwa kinachopelekea ukatili Kwa watoto na kushidwa kuendelea na Masomo.

Akizungumza katika kilele cha Juma la Elimu inayoadhimishwa Kila mwaka katika Shule ya Secondary Ufana ambapo amepongeza uongozi wa Shule hiyo Kwa kuanzisha jukwaa hilo huku akiwataka Wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto hasa wanaoishi nje na Nyumbani na kuwaagiza Watendaji na Maafisa elimu ngazi ya kata kujuwa utaratibu unaotumika katika upangishaji wa nyumba Kwa wanafunzi.

Mwl.Mugisha Galibona amesema "natoa wito Kwa Viongozi wakiwemo Maafisa Elimu kata kuweka utaratibu wa kufahamu nyumba zinazopangishwa na wanafunzi kama zinaendana na yanayofanyika huko maana isije ikawa mzazi anachangia na huku moto anachukuwa hela Kwa mtu mwingine matokeo yake mtoto anaharibika"

Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Secondary Ufana Mwl.Haikasia Minja amesema Shule Juma la elimu limeanzishwa Kwa lengo la kuongeza taaluma katika Shule hiyo kwani mpaka sasa wamefanikiwa kupunguza Utoro na Wazazi kujuwa mwenendo wa tabia za watoto wao pamoja na kuongeza ushirikiano baina ya Walimu na Wazazi katika Kushiriki kuchangia maendeleo ya Shule hiyo.

Aidha Mwl.Haikasia Minja amesema wanafunzi hupata fursa ya kufanya maonyesha ya kiataluma pamoja na Masomo ya stadi za Maisha na ujasiria Mali kwani wanafunzi hushiriki kutengeneza sabuni pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana ukatili wa kijinsia.

Aidha Mwl. Minja amesema Kupitia Juma la elimu Shule imekabidhiwa Baskeli 50 kutoka Kwa wadau wa maendeleo na kugawiwa Kwa wanafunzi waishio mbali huku pia Shule ikipatiwa Computer 20 pamoja na Bati 120 kwaajili ya ujenzi wa Hostel za watoto wa kike wa kidato cha Tano na sita.

Kwa upande wao Wazazi wenye wanafunzi katika Shule hiyo wamepongeza uongozi wa Shule Kwa juhudi zao za kuinua Taaluma Kwa watoto wao kwani Kupitia Juma la elimu Wazazi wametambua wajibu wao wa ushiriki katika kuboresha miundombinu ya Shule ya Secondary Ufana.

Hata hivyo Shule ya Secondary Ufana Kupitia maadhimisho ya Juma la Elimu imefanikiwa kuwaunganisha Wazazi na uongozi wa Shule hiyo jambo liliongeza ubora wa Taaluma na kuongeza ufaulu mwaka Hadi mwaka.
Share To:

Post A Comment: