Wizara ya Fedha imeziasa taasisi za umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji ili kuchochea uchumi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamaja, amesema taasisi za binafsi na umma zinapaswa kutumia masoko ya mitaji ili kuchochea uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Kamishna Mwamaja ameipongeza Benki ya CRDB kwa mafanikio na  fedha zilizokusanywa zitasaidia kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo na yenye faida nyingi za kimazingira kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

 Benki ya CRDB imetangaza matokeo ya mauzo ya hatifungani yake ya kijani “Kijani Bond” ambayo imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 171.82 sawa na asilimia 429.55 ikilinganishwa na lengo la kupata shilingi bilioni 40 zilizopangwa awali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameelezea kuwa matokeo hayo ni kiashirio cha imani walionayo wawekezaji wa ndani pamoja na nje ya nchi.  

Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA. Nicodemas Mkama, amesema hatua hiyo ni mafaniko makubwa katika soko la mitaji.


Share To:

Post A Comment: