Mshauri Mkuu wa masuala ya kijamii kutoka Kampuni ya Shell Tanzania, Msumis M'bena akizungumza wakati akifunga mashindano yaliyo wakutanisha wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi kutoka Shule za Sekondari 15 za Mkoa wa Lindi yaliyofanyika Oktoba 2, 2023 mkoani humo.

.........................................

Na Said Hauni, Lindi.

 

TAASISI ya Young Scientits Tanzania (Yst) imewakutanisha wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi katika Shule za Sekondari (15) za Mkoa wa Lindi, lengo likiwa kuonyesha uwezo wa kimawazo katika ugunduzi na bunifu mbalimbali zitakazowawezesha kusaidia Jamii na Taifa,

Makutano hayo yaliyokuwa imeshirikisha Sekondari (15) Halmashauri za Kilwa, Liwale, Nachingwea, Ruangwa, Mtama na Manispaa ya Lindi,umefanyika ukumbi wa  Sekondari ya Wamasharaf mjini Lindi.

Akitoa taarifa wakati wa kufunga kikao cha makutano hayo,mwakilishi wa taasisi hiyo, Botgas Kamugisha alisema la mashindano hayo ni kuwawezesha wanasayansi chipukizi kukuza bunifu walizonazo kwa ajili ya kusaidia jamii na Taifa.

Kamugisha alisema katika mashindano hayo sekondari (15) kutoka Halmashauri za Kilwa,Liwale, Nachingwea ,Ruangwa.Mtama na Lindi Manispaa zimefanya vizuri katika Project zao kubuni mambo mbalimbali.

Alisema kati ya shule hizo zilizofanya vizuri ni mbili za Mkowe,Wilaya za Ruangwa na Kivinje Kilwa na kuwakilisha Mkoa wa Lindi katika madhindano yatakayofanyika Dar es Salaam, Oktoba 17,2023.

 Mwakilishi huyo alisema Sekondari ya Kivinje imeibuka mshindi kwa Project yao kuibua kinyesi cha wadudu waitwao Youth Breck Soja kutengenezea mbolea,wakati Shule ya Mkowe kugundua dawa ya kutibu maradhi ya tumbo kwa kutumia magome ya mti wa mwembe.

Naye, mshauri mkuu wa masuala ya kijamii kutoka Kampuni ya Shell Tanzania,Msumis M'bena alisema kampuni hiyo inafadhili mradi huo kuanzia mwaka 2913 lengo likiwa ni kuboresha masomo ya sayansi kwa shule za sekondari,hali inayowasaidia kuwa wabunifu na watafiti wazuri.

Akifunga kikao cha makutano ya mashindano hayo, Afisa Elimu Mkoa wa Lindi, Joseph Mabeo amewataka wanafunzi kupenda kusoma masomo ya sayansi,ikizingatia Tai linahitaji wataalamu wa kutosha kwa lengo la kusaidia nchi.

Mabeo amesema kutokana na umuhimu huo Serikali inaendelea kuweka msisitizo na fedha za kuongeza ujenzi wa Shule na maabara.

"Mwaka huu Serikali imeupatia Mkoa wetu wa Lindi Sh,5.0 bilioni kujenga Sekondari kwa masomo ya sayansi pekee"Alisema Mabeo.

Wakizungumzia ushindi walioupata,Hadija Mohamedi na Mustapha Omari, Kivinje Sekondari na Gabliel Daniel na Mary Agustine wa Shule us Mkowe wanaishukuru Taasisi ya YST kuandaa mashindano hayo kwani yanawasaidia kufikiri katika gunduzi wanazozifanya, huku wanaamini kufikia malengo yao.

Afisa Elimu Mkoa wa Lindi, Joseph Mabeo, akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo..
Wanafunzi hao kutoka shule za Sekondari 15 mkoani humo wakiwa kwenye ufungaji wa mashindano hayo.
 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: