Na John Walter-Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea  kugawa viatu kwa Wanafunzi wa shule za Msingi za Vijijini wanaotoka familia duni Mkoani humo.

Amesema hatua hiyo inaongeza hamasa kwa watoto kupenda shule na kuongeza mahudhurio.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake leo oktoba 17,2023 Sendiga amesema kampeni hiyo katika mkoa wa Manyara inaendelea ambapo shule  ya msingi Katesh A yenye mahitaji maalum nayo imepata fursa hiyo.

"Alama aliyoiacha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkoa wetu wa Manyara haitofutika, watoto waliovishwa viatu hawawezi kusahau, mungu aendelee kumbariki" alisema Sendiga

Amesema katika mkoa wa Manyara, Rais Samia ameboresha miundombinu ya Elimu kwa kujenga madarasa mapya na shule mpya maeneo mbalimbali.

Mwenyekiti wa kampeni ya Mama ongea na mwanao mchekeshaji Steven Mengere (Steve Nyerere) amesema kampeni hiyo imebeba mambo mengi katika kila nyanja kwa ajili ya kuwasaidia watanzania.

Baada ya Serikali kutoa elimu bila malipo kwa Wanafunzi kuanzia elimu ya msingi Hadi kidato Cha sita, Kutoka nyumbani mpaka shuleni 

Steve Nyerere amesema kwa mkoa wa Manyara wanatarajia kugawa viatu zaidi ya pea 2800.

Amesema serikali ya awamu ya sita imeweka miundombinu mizuri katika sekta ya elimu hivyo wanawajibu  kumuunga mkono kwa kuhakikisha watoto wanaipenda shule.

Kampeni hiyo ilianza mwaka Jana ambapo waligawa zaidi ya pea 2,000 za viatu kwa watoto katika mikoa ya Pwani wilaya ya Kibiti na mkoa wa Tabora na wilaya zake.

Share To:

Post A Comment: