Na John Walter Babati

Mfuko  wa pensheni Kwa watumishi wa umma (PSSSF), imeshiriki katika kutoa elimu juu ya huduma ya PSSSF kiganjani Kwa lengo la kurahisisha na kuwafikia  wanachama pamoja na wastaafu kuweza kuwafikia huduma hiyo.

Hayo yamesema  na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma PSSSF wakati wa maonyesho ya Biashara Katika Wiki ya Vijana Kitaifa, maadhimisho ambayo yanafanyika katika eneo la  stendi ya zamani mjini Babati mkoani Manyara.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bwana Donald Maeda amesema katika Banda la PSSSF mwanachama atapata  huduma zote za Mfuko zinazopatikana katika ofisi zote za Mfuko.

Huduma hizo ni pamoja na kupata taarifa za michango yake, kupata taarifa za mafao mbalimbali, Uhakiki wa Wastaafu pamoja na Elimu kwa Wanachama, pia Wanachama na Wastaafu wataunganishwa na huduma ya PSSSF Kiganjani.

Share To:

Post A Comment: