Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kampasi ya kivukoni jijini Dar es Salaam leo kimeadhimisha kongamano la pili la kimataifa la kitaaluma la kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, pamoja na kuzindua kitabu kinachoelezea maono na Falsafa za baba wa Taifa.

Akifungua Kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema jamii inapaswa kuzingatia Falsafa na Maono  ya baba wa Taifa ikiwemo Demokrasia, Uhuru kwa wote, Uzalendo kwa maslahi ya vizazi Vya sasa na baadaye.

Baadhi ya Wanataaluma wa ndani na nje ya nchi ikiwemo nchi ya  Ujerumani, India na Malawi wameshiriki Kongamano hilo kwa kuwasilisha mada za Taifiti mbalimbali  zilizofanywa ikiwemo eneo la Elimu, Siasa, Kilimo, Viwanda  Uongozi na Utawala bora.        

Mada Kuu ya  Kongamano hilo ni ‘Urithi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Uongozi na Maendeleo ya Jamii na Uchumi katika kipindi kipya Cha Mapinduzi ya viwanda’.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano na Masoko

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

13.10.2023

Share To:

Post A Comment: