Julieth Ngarabali, Kibaha

Zaidi ya shilingi milioni 60 zimetumika kutekeleza mradi wa maji katika shule ya sekondari ya wavulana ya vipaji maalumu ya Kibaha, mkoani Pwani, hatua ambayo imetatua tatizo la ukosefu huduma hiyo.

 Akizindua mradi huo shuleni hapo, Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya michezo yakubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe, alisema mradi huo umelenga kutatua tatizo la maji lililokuwa likiikabili jumuiya ya shule hiyo ikiwemo wanafunzi.

Alisema mradi huo umefadhiliwa na bodi hiyo kwa asilimia mia moja  kwa gharama ya jumla ya s Milioni  64,656, 520 ambapo imejumuisha uchimbaji wa kisima, ujenzi wa Tanki la aridhini lenye ujazo wa Lita laki moja Pamoja na ununuzi wa matenki 10 ya kuhifadhia maji.

"Awali shule hii iliomba ufadhili kwetu na baada ya kujiridhisha tatizo la maji lipo tulikubali na kutoa kiasi hicho cha fedha ambapo Pamoja na mambo mengine pia tumetoa fedha kujenga uzio kuzunguka kisima, minara ya kuhifadhia matenki Pamoja na miundombinu ya usambazaji wa maji"alisema

Aidha alitoa wito kwa wanafukaika wa mradi huo ikiwemo wanafunzi kutunza miundombinu ya mradi hatua itakayo saidia kudumu na kusaidia vizazi vijavyo.

"Ni matumaini yetu kuwa mradi huuutawezeaha upatikanaji wa uhakika wa maji Kwa muda wote hivyo tunaomba kila mwanajumuiya wa shule ya sekondari Kibaha awe mlinzi na mtunzaji wa mradi huu ili uweze kusaidia vizazi vijavyo"alisema 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la elimu Kibaha,Robert Shilingi, aliishukuru bodi hiyo Kwa ujenzi wa mradi huo na kwamba mradi huo utasaidia kukuza kiwango Cha ufaulu Kwa wanafunzi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

"Licha ya kutatuliwa tatizo la maji, bado yapo maeneo yanachangamoto ikiwemo jiko letu la gesi kuwa chakavu, pamoja na kwamba serikali imekuwa ikitoa fedha,tutafarikika kuona wadau wengine wanajitokeza kusaidia  kuboresha mradi huu hatua itakayo saidia kuondokana na nishati ambazo sio rafiki wa mazingira"alisema

Mwisho 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: