Na John Walter-Babati

Mwenge wa uhuru umekamilisha mbio zake mkoani manyara katika Halmashauri ya mji wa Babati na kukagua, kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.16.

Mwenge huo ukiwa mjini Babati umezindua vyumba vitano vya madarasa, ofisi na matundu 6 ya vyoo katika Shule ya Msingi Hangoni, Mtaa wa Majengo, Kata ya Babati uliogharimu shilingi Milioni 135,122,000.00.

Aidha Mwenge ulipita katika kata ya Mutuka na kuweka jiwe la msingi  ujenzi wa  box culvert  ambapo chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa mwaka wa fedha 2023/2024 zitajengwa box culvert 3 katika barabara za BABATI – MUTUKA,SAMRE (SAWE), MABOA na pipe culvert 4 katika barabara ya DAGHAILOI - SINGU  ambapo utagharimu kiasi cha shilingi 459,848,000.00 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu (Tozo ya Mafuta).

Mradi mwingine ni wa Zahanati ya kijiji cha Imbilili ambao  ulianza mwezi Juni, 2023 na ujenzi upo hatua ya ukamilishaji na hadi sasa ujenzi umegharimu kiasi cha Tsh. 51,797,000.00 

Maktaba katika shule ya Sekondari Sigino ambapo Mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 92,387,000.00.

Mradi mwingine uliotembelewa na Mwenge ni wa Kikundi cha Vijana cha Kalakasai  ambao Kikundi walifanikiwa kupata Mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani kwa vipindi tofauti Mwaka 2016/2017 Mkopo wa Tshs. 2,000,000, Mwaka 2017/2018 Mkopo wa Tshs. 3,000,000 na Mwaka 2020/2021 Mkopo wa Tshs. 2,000,000 na Kufanya Jumla ya Mkopo uliotolewa kwa Kikundi kuwa Tshs. 7,000,000 na kimefanikiwa kurejesha mkopo wote. 

Aidha ameweka jiwe la msingi ujenzi wa tenki la maji lililopo Mtaa wa Maisaka A, Kata ya Maisaka, Halmashauri ya Mji wa Babati unaosimamiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Babati (BAWASA) utakaogharimu shilingi bilioni 1,426,033,860.57 .

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim amempongeza mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange na wataalamu, kwa kusimamia vyema fedha za serikali akisistiza utunzaji wa nyaraka za miradi na kuikamilisha mapema ii itoe hufuma kwa wananchi.

Kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa uhuru mwaka  2023 "Tunza Mazingira,Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai, kwa Uchumi wa Taifa"

Share To:

Post A Comment: