Zaidi ya wanachama 6 wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kata ya Machame Kaskazini wilayani Hai wamerudisha kadi zao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM huku wengine 18 wakijiunga na CCM na kubainisha kuwa ni kutokana na juhudi za maendeleo zinazofanywa na mbunge Saashisha Mafuwe pamoja na Chama cha mapinduzi kupitia ilani yake ya uchaguzi.

Hayo yamejiri katika ziara ya mwenyekiti wa UWT wilaya ya Hai Happiness Eliufo ambapo mbali na kuwapokea wanachama hao pia amewaomba wanachama wa CCM kata ya machame kaskazini kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan ambazo ndio ilani ya chama Cha mapinduzi ambapo kupitia ilani hiyo kumèpelekea wanachama wapya ndani ya chama pamoja na jumuiya ya wanawake UWT.

" Hongereni sana mliokuja leo kujiunga na CCM, hongereni ninyi mliorudisha kadi za vyama vingine na hapa mmesema ni kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM pamoja na maendeleo mnayoyaona, na sisi tunasema tutafanya kazi kubwa ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana ila na ninyi muungeni mkono mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mbunge wetu Saashisha Mafuwe  na chama chetu cha mapinduzi". Alisema Happyness Eliufoo.

Sambamba na hayo mwenyekiti huyo wa UWT amewataka jumuiya ya wanawake kuwa na mshikamano katika kukijenga na kukiimarisha chama huku pia akiwasihi wanawake kujitokeza kwa wingi mwaka 2024 katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya kata.

Hata hivyo  UWT kata ya machame kaskazini hawakusita kutoa pongezi zao za dhati kwa UWT ngazi ya wilaya kwa jinsi ambavyo imekuwa ikionesha uhai wake pamoja na kutoa hamasa kwa wanachama wake pamoja na kusimama kidete katika kushughulikia changamoto mbalimbali katika kata ikiwemo vitendo vya kikatili vinavyotokea ndani ya kata.

Share To:

Post A Comment: