Kilio Cha muda mrefu juu wa upungufu wa madawati 96 ndani ya shule ya msingi ya lemara kimetatuliwa hii leo na Diwani wa Kata hiyo ya lemara Naboth Silasie

Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo kwa uongozi wa shule ya msingi lemara ametumia wasaa huo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uongozi thabiti kwa Kuendelea kutengenezea mazingira mazuri na mashirika mbalimbali kwani Kupitia uongozi wake wameweza kupata wafadhili kutoka NMB BANK  ambao wametoa mchango wa madawati Mia Moja katika shule ya msingi lemara.

Amesema kuwa wapo wanaolaumu wanafunzi hawafaulu vizuri lakini wanafunzi wanakuwa wamekaa sita au Saba kwenye dawati Ambapo inapelekea wanafunzi kushindwa kumsikuliza mwalimu vizuri na badala yake wanasumbua na kusukumana darasani

Sambamba na hilo amesema wanafunzi watakaa vizuri darasani kwani uwepo wa madawati hayo mapya yanakwenda kupunguza msongamano madarasani na wanafunzi watakaa wawili hadi watatu

Nae Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Itika swalehe kirango amesema lemara inayoonekana Sasa sio lemara ya miaka ya nyuma kwani kilio Chao kama Walimu ni upungufu wa  madawati na Sasa Diwani ameweza kutatua kilio hicho.

Amesema shule ya msingi lemara ilikuwa na upungufu wa madawati 96 na Kupitia juhudi za Diwani wameweza kupata madawati 100 pamoja na ukarabati wa madarasa 

Pia amewaomba wazazi kumuunga mkono Diwani kwa kuwasimamia watoto wao kusoma kwa  pindi wawapo nyumbani Ili jitihada za Naboth zisijekuishia kwenye kuleta madawati tu kwani kwa Sasa wanafunzi watakaa kwenye madawati imara, wataandika vizuri na watakaa kwa nafasi.

Nae Mwenyekiti wa lemara Charles kiumba amesema uwepo wa madawati hayo mapya ni kuonyesha kuwa Serikali inafanya kazi kwani shida ya madawati kwa Sasa kwa shule ya msingi lemara imetatuliwa.

Nao wazazi waliojitokeza kushuhudia zoezi la kukabidhiwa kwa madawati hayo wamemshukuru Diwani wa Kata hiyo kwani wao kama wazazi hawakuwa na uwezo wa kuchangia madawati hayo yote Kutokana na ugumu wa kimaisha



Share To:

Post A Comment: