Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea na kukagua utekelezaji wa  Mradi wa Maji Mkunywa uliopo Kata ya Madibira  Wilayani Mbarali.

Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Mahundi amesema kuwa mradi huo, unagharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 847 ambapo mpaka sasa mkandarasi amelipwa kiasi cha fedha shilingi milioni 128 kama malipo ya awali. Pia,utekelezaji wa mradi ulianza mwezi Septemba, 2022 na ukamilishaji wake ulitarajiwa ukamilike Mwezi Machi, 2023 kulingana na Mkataba.

Mhe. Mahundi amesema Mkandarasi ameshindwa kukamilisha utekelezaji wa mradi huo sanjari ya kuongezewa muda wa mkataba na ameweza kutoa maagizo kwa meneja wa RUWASA MKOA kuwa asimamie taratibu zote  za kimkataba ili mradi huo uweze kutekelezwa kwa kutumia utaratibu wa force account.

Naye Mbunge Mteule wa Jimbo la Mbarali Mheshimiwa Bahati Ndingo ameishukru Serikali kwa utekelezaji wa miradi ya Maji kwenye Jimbo la Mbarali na kusisitiza kuwa Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Mkunywa aondolewe kwasababu wananchi wa vijiji vya Ikoga, Mkunywa, Chalisuka, Mahango na Iheha wanakosa huduma ya maji kwa uzembe wa mkandarasi.Share To:

Post A Comment: