Na John Walter-Mbulu

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, ameanza utaratibu wa kupita kwenye idara ya Afya kukagua hali ya utoaji huduma katika hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati katika wilaya hiyo.                        

Katika ukaguzi huo mkuu wa wilaya anaangalia hali ya upatikanaji wa Dawa, mahudhurio ya watumishi, utekelezaji wa mpango kazi wa afya, upatikanaji wa huduma wezeshi kama maji na mengine, pamoja kuzungumza na wagonjwa wanaohudumiwa katika maeneo hayo.                        

Hata hivyo ameonyesha kuridhishwa na huduma zinazotolewa akiwapongeza watumishi na wahudumu na kuwahimiza kuchapa kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi ya Taaluma na utu.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia kuwezesha na kuimarisha mazingira bora ya utoaji wa Huduma za Afya.                    

Mkuu wa wilaya  aliwataka wananchi wasisite kutoa taarifa pindi wanapopata changamoto katika maeneo ya huduma za Afya.                      

Share To:

Post A Comment: