Katibu wa NEC,  Itikadi na Uenezi CCM Taifa,  Ndg. Sophia Mjema amewataka wanachama wa CCM wanaoutaka ubunge na udiwani kuwa na subira hadi 2025.

Amesema hayo Oktoba 5, 2025, alipozungumza katika mkutano wa viongozi na watendaji wa CCM mkoani Songwe.

Amesema kwa sasa hadi 2025, Chama kinawatambua wabunge na madiwani waliopo, hivyo waendelee kuungwa mkono katika kazi wanazozifanya hadi kipindi chao cha uongozi kitakapomalizika.

Amesema wanachama wanaojipitishapitisha kwa malengo ya kuutaka ubunge na udiwani kabla ya wakati, watashughulikiwa.

Ndg. Mjema amesema, “ukitamani uongozi subiri 2025 sasa hivi waachwe viongozi waliochaguliwa  wamalizie kazi tuliyowatuma, muda ukifika utaomba ila kwa sasa tunataka mshikamano, nyumba ni maelewano, yasipokuwepo hakuna maendeleo."

Mwenezi Mjema yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Songwe yenye lengo la kukiimarisha na  kukijenga Chama, akiwa ni Mlezi wa Mkoa huo.


Share To:

Post A Comment: