Na Imma Msumba; Arusha 

Chuo Cha uhasibu Arusha kimezindua kamati ya ushauri wa kisekta (Industrial Advisory  Committee) itakayoboresha mitaala sambamba na kuleta  mabadiliko makubwa katika kuzalisha wataalamu bobezi katika fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

Akizingumza wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo chuoni hapo ,Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho ,Dk Mwamini Tulli amesema kamati hiyo ndiyo itakayokua mshauri na kiunganishi  kikubwa katika kuhuisha mitaala iliyopo, na kuandaa mitaala mipya Ili wataalamu wanaosoma fani mbalimbali chuoni hapo waweze kutoa usuluhishi katika changamoto za kisekta .

Dk  Tulli amesema  kamati hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HEET wenye  lengo la kujenga daraja la kudumu kati ya chuo hicho na wadau hao katika sekta mbalimbali ambazo zitapokea watalaamu wanaoandaliwa katika fani mbalimbali zikiwemo uhasibu na fedha, benki  ,uchumi,kodi ,Tehama 'utalii usimamizi wa biashara pamoja na ukaguzi wa fedha. 

"Kamati hii ni muhimu sana kwetu Sisi katika kutushauri na kutuongoza kuhusu jinsi tunavyoweza kutoa elimu inayokidhi mahitaji ya soko la ajira na kamati hiyo itakuwa jukwaa la majadiliano, mawazo na ubunifu unaolenga kuboresha programu za masomo na kuweka mwelekeo  sahihi."amesema Dk Tulli. 

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Prof.Eliamani Sedoyeka amesema chuo kitaendelea kufanya tafiti na mabadiliko ya mitaala ili kuendana na ukuaji wa Sayansi na Teknolojia nchini na kutoa wataalamu bobezi.

Prof . Sedoyeka amesema ,tukio hilo  ni moja kati ya majukumu ya msingi kwani chuo hicho kina wajibu wa kutoa mafunzo,ushauri wa kitaaluma na kufanya tafiti hivyo majukumu hayo hayawezi kuwa na uhalisia na kwenda kutoa majawabu katika maeneo mbalimbali bila  ya kuwa na muongozo  dhabiti wa kufanya hivyo na kamati hiyo ndo itakuwa kiunganishi kikubwa kati ya wao chuo na sekta mbalimbali. 

"Na tunategemea baada ya bodi hiyo kuanza kufanya kazi itatupa mrejesho na miongozo ambayo itawasaidia wao kuweza kufanya kazi vizuri zaidi katika kuboresha mitaala mbalimbali ambayo  itaendana na soko la ajira"amesema .

Aidha amefafanua, chuo hicho ni kati ya vyuo ambavyo vimeweza  kupata mradi wa  HEET  na wameshaanza kupokea  dola milioni 21 ,hivyo wanamshukuru  Rais Samia Samia kuona umuhimu wa kuwapatia mradi huo na tukio hilo  la  leo ni kati ya utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha vyuo vinajengewa uwezo na vinajipanga  kutoa mazao bora  yanayoendana na mahitaji ya mazao ya soko.

"Sisi kama chuo tunahitaji  kutoa watu wanaoendana na mahitaji ya sasa na uzinduzi wa kamati hii ndo inaenda kujibu mahitaji hayo kwani wengi wa wajumbe wa kamati hiyo wanatoka maeneo mbalimbali ambayo kila mmoja kwa nafasi yake ataleta  mchango  pekee katika nafasi zao."amesema .Prof .Sedoyeka. 

Nao Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo Elias Kajiba  kutoka chama cha waajiri Tanzania (Ate ) na  Liliani Riwa wamesema kwa pamoja watahakikisha wanatekeleza  majukumu ya chuo hicho kwa kutoa ushauri na  hatimaye kuweza kutoa late wanaokidhi  soko la ajira  na kuweza kuajirika kwa urahisi.

Hata hivyo uwepo wa kamati hiyo utasaidia kuleta mabadiliko makubwa hapa nchini katika utoaji wa Elimu ambapo itagusa wanafunzi na kugusa matatizo ya jamii yanayowazunguka .


Share To:

Post A Comment: