Timu 41 za soka Wilayani Longido Mkoani Arusha zimethibitisha kushiriki mashindano ya Kombe la Kiruswa Jimbo Cup na juzi uzinduzi wa Michunano hiyo ulifanyika kwa pambano kati ya timu za Namanga Veterani dhidi ya Loiboni fc kupambana katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa polisi Longido.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Wilayani Longido {LDFA},Obeid Joseph amesema kuwa mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Mbunge wa Longido Dkt Steven Kiruswa na kuratibiwa na kusimamiwa na Chama hicho yatapangwa katika makundi matano na yatachezwa kwa mtindo wa ligi katika viwanja mbalimba wilayani Longido.

 

Joseph alisema kuanzishwa tena kwa mashindano hayo ambayo yalisimama wa miaka miwili kwa sababu mbalimbali ni fursa kwa vijana wa wilaya hiyo ili waweze kuonyesha vipaji vyao na hatimaye waweze kuajiliwa katika timu kubwa za ndani na nje ya Nchi.

 

Alisema na kuwataka vijana kujitokeza kushiriki ligi hiyo kwa kuwa kuna weza kuwaondoa katika matukio yasikuwa mazuri kwa jamii ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na kujihusisha na matukio ya uhalifu wa jamii ya Longido.


Akizungumza katika Uzinduzi huo juzi,Kiruswa alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa endelezu kwa miaka yote na ameahidi donge nono wa washindi na ameahidi kuboresha michezo mingine wa vijana wa Longido.

 

Kiruswa alisema kutofanyika kwa miaka miwili ni kutokana na ugonjwa wa Uviko 19 mwaka juzi na mwaka jana Jimbo la Longido lilikumbwa na ukame ndio maana mashindano hayo hayakufanyika lakini kuanzia mwaka huu mashindano hayo yatakuwa endelevu.

‘’Nawataka Vijana kujitokezeni kushiriki mashindano hayo ya mwaka huu kwani donge nono kwa washindi litatoa na zawadi hiyo ntasema baadae’’alisema Kiruswa

 

Naye Mgeni Rasmi katia uzinduzi wa mashindano hayo,Mwamvinta Okengwa ambaye ni Afisa Michezo Mkoa wa Arusha alimsifu Mbunge wa Jimbo la Longido kwa kubuni kuanzishwa kwa mashindano hayo na kusema kuwa hiyo ni chachu ya kuendeleza michezo katika wilaya za kifugaji.

 

Okengwa alisema kuwa wilaya ya Longido na Ngorongoro ni wilaya za kifugaji hivyo zinahitajika kufanyiwa kazi ya ziada kuanzishwa mashindano ya soka na michezo mingine ili kuwahamashisha vijana wa jamii hiyo kushiriki michezo.

 

Alisema hatua ya timu zote 41 kupewa seti moja ya jezi na mpira mmoja ni hatua tosha ya kumvuta kijana kushiriki mashindano hayo hivyo aliwaomba wadau wengine kuiga mfano wa Mbunge Kiruswa katika majimbo wanayoongoza kwa sera ya Chama Cha MapinduziCCM} inaeleza wazi juu ya kuinua soka.

 

Katika mchezo wa uzinduzi timu ya Laiboni ya Mjini Longido ilifanikiwa kuibuka washindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Namanga Vaeterani na kufanikiwa kubeba ngao na kuvalishwa medali ya dhahabu.

Share To:

Post A Comment: