Na Denis chambi, Tanga.

CHAMA cha ACT-WAZALENDO  jimbo  la Tanga pamoja  na  wakazi  wa  jiji  la Tanga , leo  agosti 11 wamejitokeza  kwa  wingi  kuchangia  Damu Salama  kwaajili  ya  wagonjwa  wanaopatiwa huduma  kwenye  Hospitali  ya Rufani  mkoa wa Tanga  Bombo,

Uchangiaji  huo  wa Damu  Salama umeenda sambamba  na  zoezi  la uhamasishaji kwa  jamii juu ya  faida za uchangiaji wa Damu Salama  ikiwa  ni  kuelekea  maadhimisho  ya siku  ya Vijana   Duniani  yanayofanyika kila    Agosti  13 .

 Mwenyekiti  wa Jumuiya  ya  Wanawake  chama hicho  Mkoa  wa Tanga  Rehema Mohammed  aliwaambia   Waandidhi wa Habari  kuwa  Chama  hicho  kinatarajia  Kufanya  kongamano  la  Vijana  agosti 13 ikiwa  ni Kilele cha maadhimisho  ya  Siku  ya Vijana Duniani  hivyo  katika  kuelekea  siku  hiyo wameona  nivyema  kuokoa Maisha  ya watu wengine,

‘’Kwakuzingatia  umuhimu  wa   Damu  hususani  kwasisi  wanawake  chama  chetu  kimeona  ni  vyema  kuokoa maisha  ya  watu  wengine na  tunaendelea  kufanya  hamasa  hii  kwa  Wakazi  wote  wa Tanga  kujitokeza  kwa  wingi  kwenye  uchangiaji  wa Damu’’ Alisema Rehema

Sambamba  na hayo  Rehema  alisema  kabla  ya maadhimisho  hayo  wanatarajiwa  kufanya  matukio  mbalimbali ikiwamo  kufanya  mikutano  ya  Hadhara na  makongamano yakuwaelimisha  Vijana  juu  Mambo  mbalimbali  ya Nchi yao  ikiwamo  Uzalendo  kwa  Taifa.

Kwaupande  wake  katibu wa  ngome ya  Vijana  ACT-WAZALENDO   jimbo  la Tanga  Kassimu  Hassan aliwashukuru  Wananchi  kwakuitikia  wito wakuchangia  Damu,

‘’Tunawashukuru  wakazi  wa Jiji la Tanga kwakujitokeza kwa wingi  kuchangia  Damu  tunawaomba  waeendelee kuwa  Wazalendo  kwakuhamasishana  kuchangia  zaidi  ili tuokoe  maisha  ya  wengine  lakini  hata  sisi pia  ni  wagonjwa watarajiwa’’ Alisisitiza Kassimu

 Mwenyekiti  wa Jumuiya  ya  Wanawake  chama hicho  Mkoa  wa Tanga  Rehema Mohammedakizungumza na wanahari kuhusu zoezi hilo la uchangiaji damu lililofanyika katika ofisi za chama hicho .


Wataalamu wa maabara kutoka katikahospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo wakitoa elimu ya uchangiaji damu  wanachama wa ACT Waalendo waliojitokeza katika kushiriki katika zoezi hilo
 
Baadhi ya wanachama wa chama cha ACT Wazalendo waliojitokeza katika ofisi za chama hicho  kuchangia damu salama leo augost 11,2023.

Share To:

Post A Comment: