NA DENIS CHAMBI,  TANGA.

BENKI ya NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa wadau wakiwemo  walimu wa shule za msingi na sekondari ambapo imekuja na huduma ya Mwalimu Spesho yenye lengo la kuwawezesha na kuwainua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa za mikopo kwaajili ya biashara,  kilimo na ada.

Zaidi ya walimu 300 kutoka katika shule mbalimbali za msingi na sekondari mkoani  wa Tanga  wameshiriki  warsha iliyoandaliwa na Benki hiyo ya NMB kanda ya Kaskazini kwa lengo la kuwapa elimu juu ya huduma na fursa mbalimbali zikiwemo elimu ya kifedha,  na elimu ya  bima.

Akizindua Warsha hiyo mkuu wa wilaya Tanga James Kaji ameipongeza Benki hiyo kwa kundelea kuboresha huduma zake kwa wadau wa hususan wa  serikali akiwataka walimu kutumia fursa  za mikopo  zinazotolewa kwaajili ya kuwainua wateja wake  hasa kiuchumi,   kielimu ,  kwenye sekta ya kilimo akiwataka kuachana na  mikopo umiza ambayo wamekuwa wakiipata sehemu nyinginezo.

Aidha Kaji alisema kwa kuwainua kiuchumi walimu itawasaidia pia  kuwawezesha hata kiutendaji  katika majukumu yao ya kiufundishaji hatua ambayo itasaidia kuwaandaa wanafunzi bora kitaaluma na maadili mema.

"Nitoe pongezi kubwa sana kwa Benki ya NMB kwa kuandaa kongamano hili kila mwaka kwa walimu imetoa msisitizo mkubwa na kuwawezesha walimu,  wazo la kuwafikia walimu hususan katika kuwawezeaha kimikopo  ni zuri na la kuigwa ,  na nyinyi walimu onyesheni jithada na uwezo wenu katika  kuchangamkia na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana" 

"Walimu wengi katika shule zetu za msingi na sekondati wengi wao walikuwa wakijiingiza katika mikopo umiza ambayo imefanya wanashindwa  kutekeleza majukumu yao ya kila siku lakini kwa fursa hizi zinazotolewa,  na tumeshuhudia wengi wao  kutokana na mikopo inayotokana na NMB wameboresha maisha yao kutokana na huduma  jinsi ambavyo wameweza kuinuka kimapato na kuboresha maisha yao ya kila siku" alisema Kaji.

Awali akizungumza  mkuu wa kitengo ya Bima  kutoka benki ya  NMB kanda ya kaskazini Martin Masawe kwa niaba ya afisa biashara na wateja binafsi amesema kuwa walimu wana nafasi kubwa ya kunufaika na  huduma mbalimbali wanazozitoa  huku wakiwa na lengo la kuwafikia walimu wote nchi nzima.

"Tumekuwa tukitoa elimu ya kifedha,  elimu ya bima  na elimu mbalimbali za kujipangilia kimaisha kwa walimu,   bila mwalimu pengine sisi tusingekuwepo hapa  na umuhimu wa walimu katika benki yetu ni jambo kubwa na la umuhimu sana tumekuwa tukifanya hivi kila mwaka na tumepanga kuwafikia walimu wote nchi nzima na kwa mwaka huu tunategemea kuwafikia walimu 9000 katika wilaya na mikoa mingi zaidi sambamba na kutoa elimu kwa walimu wote" alisema Massawe

"Benki ya NMB iliangalia ni kitu gani cha kipekee ambacho anaweza kupata mwalimu kutoka  kwetu kwahiyo tulitengeneza masuluhisho kulingana na maisha yao ambapo tunayoa mikopo  kwaajili ya elimu pale wanapotaka kujiendeleza  au mtoto wake anaweza kupata mkopo wenye riba nafuu ya 9%,  tunatoa mikopo ya kilimo ,  tunatoa pia mikopo kwaajili ya vyombo vya usafiri kwaajili ya kujiongezea kipato zaidi ya kile ambacho anakipata mwalimu" alisema Massawe

Baadhi ya  walimu akiwemo Coletha Joseph na Maurus  Ndunguru ambaye ni kaimu afisa elimu wa halmashauri ya jiji la Tanga  wameishukuru na kuipongeza Benki hiyo  kupitia mikopo na huduma ambazo wanazipata zitakazowasaidia kuwainua kiuchumi na kuwapa fursa ya kujiendeleza kimasomo na katika maisha ya kawaida.

"Tunaishukuru sana Benki ya NMB kwa kutuona na kutuletea huduma mbalimbali hasa ya mikopo ambayo itatusaidia kutuongezea kipato nje ya kazi yetu tutakwenda kuwaelimisha na wenzetu juu ya fursa hizi zinazopatikana ili  waweze kuzitumia na kusaidia kuongeza kipato  kwa ujumla " alisema Coletha.

"Huduma hizi wanazozitoa benki ya NMB ni nzuri zitaboresha miasha ya walimu kwasababu tumekuwa tukizunguka sana kwenye mambo ya mikopo ambayo inaumiza wakati mwingine lakini kwa kuja kwao NMB hapa kutawasaidia sana walimu" alisema Ndunguru.
 
  Mkuu wa wilaya ya Tanga  James Kaji akizungumza mara baada ya kufungua washa ya kuwapa elimu ya fedha walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani Tanga iliyoandliwa na benki ya NMB  iliyifanyika Augost 8,2023  katika ukumbi wa Tanga beach.
Mkuu wa kitengo ya Bima  kutoka benki ya  NMB kanda ya kaskazini Martin Massawe akizungumza katika warsha hiyo.
Baadhi  ya walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka wilaya mbalimbali mkoani Tanga wakiwa wanafwatilia elimu ya fedha inayotolewa na benki ya NMB katika ukumbi wa mikutano wa Tanga Beach.
Share To:

Post A Comment: