Na; Elizabeth Paulo, Dodoma


Kijana Christopher Makotwe ni mnufaika wa mikopo ya asilimia 4 inayotolewa na serikali kwa vikundi vya vijana.


Anasema Kikundi chao kina jumla ya vijana wa tano (5) wakiwa na Kampuni inayoitwa TUSUKUME GROUP wanaojihusisha na uangulishaji wa mayai/ Wasambazaji na wauzaji wa Vifaranga aina zote yaani Vyakula vya Mifugo, Chanjo & Madawa, Usimamizi wa Miradi, Ushauri wa Kilimo na Ufugaji Pamoja  na Mbolea.


Christopher ni Mwenyekiti wa TUSUKUME GROUP Anasema ni vijana wajasiriamali tuliopo Kikuyu Dodoma ni wanufaika wa asilimia 4 za mkopo wa halmashauri ya jiji la Dodoma ambao wametuwezesha kukuza Mradi wetu.

Amesema hayo leo katika sherehe za maonesho ya nanenaene kanda ya kati katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma alipotembelewa na mgeni wa siku na kuelekea vitu wanavyojihusisha navyo kama kikundi.

Anasema“Tuna mashine za kuzalisha vifaranga elfu 10,000, Tumetengeneza mnyororo wa thamani wa kuku kwasababu tunazalisha vifaranga na tunatengeneza chakula cha kuku kwa kutumua mashine inayorahisisha.”Amesema Makotwe


Amesema wamekua wakipata manufaa mbalimbali ikiwemo uuzaji wa chakula cha kuku Takribani mifuko 240 kwa mwezi huku wakiuza vifaranga zaidi ya elfu 2000 kwa mwezi na kusema wanapata manufaa huyo kupitia serikali ya awamu ya Sita kuona vijana ndio Nguvu kazi ya Taifa.


Aidha Ameiomba serikali kuwatafuta vijana wengi ili kupatiwa mafunzo ya ufugaji bora na kuongeza vijana wengi kujiajiri kupitia sekta hiyo ya ufugaji wa kuku.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi Mh. Donard Megitii na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa amewapongeza vijana hao kwa kujipatia ajira hiyo huku akiwataka kuongeza bunifu zingine ili kuondokana na kufuta kabisa dhana ya uagizaji wa vyakula nje ya nchi na kuongeza bunifu katika sekta hiyo.

Katika picha ni Christopher akikabidhi zawadi ya kuku kwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Ccm Taifa Mh. Donard Megitii.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: