MBUNGE wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi ametembelea ujenzi wa Chuo cha VETA kinachojengwa katika halmashauri ya wilaya ya mlimba mkoani Morogoro ambapo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha Sh Bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi huo.


Kunambi ametoa shukrani hizo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa chuo hiko ambapo tayari mafundi wameshaanza hatua za awali za kusafisha eneo hilo kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mchombe ambao ujenzi wa chuo hicho unatekelezwa ndani ya eno hilo, Kunambi amesema kukamilika kwa chuo hiko kutakua ni historia kubwa na Rais Samia kwa wananchi wa Mlimba.

" Kwa hakika Rais Samia ameweka historia kubwa kwa wananchi wa kata ya Mchombe na Jimbo letu la Mlimba. Uwepo wa Chuo hiki ambacho kinaweza kuchukua hadi wanafunzi 1,000 ni faida kwetu kielimu lakini pia kiuchumi.

Ni kazi kwetu kuhakikisha tunamuunga mkono Rais wetu kwa kuja kujifunza fani mbalimbali hapa pindi chuo kitakapokamilika. Na kama mnavyojua VETA haiangalii umri wa mtu, yeyote mwenye kutaka ujuzi aje hapa. Ni fursa kwetu," Amesema Kunambi.

Ujenzi wa awali wa chuo hicho unatarajia kukamilika ndani ya kipindi cha miezi sita ambapo takribani majengo tisa yanajengwa kwa ajili ya kuanza kutoa elimu na ujuzi wa fani mbalimbali.
Share To:

Post A Comment: