MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani ,amekabidhi Printer pamoja na computer kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi katika shule ya Sekondari Disunyara, iliyopo Kibaha Vijijini.

Aidha amekutana na Baraza la UWT Wilayani humo, ambapo ambapo amechangia kiasi cha sh.milioni mbili na tofali 1000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi na kuwapatia viongozi wa wilaya cherahani 3 na kila kata kuipatia cherehani moja kwa kata zote 14.

Akiwa kwenye ziara yake wilaya ya Kibaha Vijijini ,amepokelewa na Viongozi wa UWT wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti Leila Hamoud Jumaa na Katibu wa UWT Wilaya Nuraty Mkandawile.

Hata hivyo,Mgalu aliwakumbusha viongozi wa UWT kuendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Vilevile amezungumzia uwepo wa mikutano ya hadhara, kuzungumza na wananchi katika ngazi mbalimbali, ikiwa na dhamira ya kupokea changamoto zao kisha kupatiwa ufumbuzi.

Katika ziara hiyo, Mgalu ametembelea vikundi vya wajasiriamali vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri , ikiwemo kikundi cha Honest Best kinachojihusisha na uuzaji wa unga na nafaka, kikundi cha vijana Kilangalanga kinachojihusisha na utengenezaji wa sabuni za maji , pilipili za kusindika na mikeka ya kushona .

Mgalu amekiwezesha kikundi cha Amani sh.720,000 ili waweze kununua bati 40 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wao.

Pia mbunge huyo ametembelea na kukagua mradi wa Boost wa madarasa matatu, matundu ya vyoo matatu na shimo moja katika shule ya msingi Kilangalanga wenye thamani ya Tsh. 71.4 milioni .

"Napongeza juhudi zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kazi kubwa anayofanya ya kuelekeza fedha nyingi za maendeleo katika maeneo mbalimbali Mkoa wa Pwani na nchi kwa ujumla "
Share To:

Post A Comment: