Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye mkutano Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambao umefanyika leo Julai 5,2023.

                Na Mapuli Misalaba, Shinyanga                                                               

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameyakumbusha mashirika yasiyo ya kiserikali NGO's yaliyopo mkoani hapa kuhakikisha yanaendelea kutekeleza miradi inayolenga kulinda na kuheshimu maadili, mila na desturi za kitanzania kwa ustawi wa Taifa.

Ameyasema hayo leo Jumatano Julai 5,2023 wakati akifungua mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Shinyanga, kwa lengo la kutambua mchango wa mashirika hayo pamoja na  kufanya majadiliano kuhusu ufuasi mzuri wa sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

RC Mndeme amesema serikali haitosita kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa shirika lisilo la kiserikali ambalo litabainika kwa makusudi kujihusisha na miradi ambayo inakiuka maadili, mila na desturi za Kitanzania.

RC Mndeme ametumia nafasi hiyo kuwaelekeza wataalam wa serikali wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuhakikisha wanaimarisha uratibu kwenye mashirika hayo ili kuepuka mrundikano wa mashirika yanayofanya kazi moja katika eneo moja.

Aidha, akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa NGO’s katika Mkoa wa Shinyanga Bwana Venance Muzuka ameiomba serikali ya Mkoa kuhakikisha inaendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki ya utendaji kazi kwa mashirika hayo, huku akiahidi kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria, miongozo na taratibu za nchi.

Katika mkutano huo wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanatekeleza majukumu yake Mkoani Shinyanga pamoja na mambo mengine wameadhimia mambo mbalimbali ikiwemo serikali kufanya ufuatilia kwa lengo la kutambua uhai wa mashirika yaliyopo ili yaweze kutoa mchango wa maendeleo Mkoani Shinyanga.

Wameadhimia pia kuwa na vikao endelevu vya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za NGO’s

Pia wameadhimia kuwa, wasajiri wa NGO’s katika Halmashauri zote Mkoani Shinyanga kuziunganisha NGO’s kubwa na mashirika madogo ili kujengeana uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha wameadhimia kuwa na semina za mara kwa mara baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuendelea kujengeana uelewa, huku wakiliomba jeshi la Polisi kitengo cha dawati la jinsia kuweka mazingira rafiki kwa watoto wakati wa kupokea na kusikiliza kesi mbalimbali ikiwemo kesi za ukatili pamoja na migogoro ya kifamilia.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye mkutano Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambao umefanyika leo Julai 5,2023.

Msajili wa mashirika, afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akitoa semina  kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.

Msajili huyo wa mashirika Bwana Ngwale  ameelezea mambo mbalimbali ikiwemo sera na sheria zinazosimamia uratibu wa mshirika yasiyo ya kiserikali, taratibu za usajiri wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na maudhui ya kanuni ya sheria ya NGO’s.

Mwakilishi wa NGO’s katika Mkoa wa Shinyanga Bwana Venance Muzuka akizungumza kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.

Afisa elimu na mawasiliano kwa mlipakodi kutoka TRA Mkoa wa Shinyanga Bi. Semeni Mbeshi akielezea mambo mbalimbali ikiwemo namna ya mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali kulipa kodi ambapo amesema mashirika yanawajibu wa kufuata sheria zote za mlipa kodi.

Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bwana Donasian Kessy akizungumza kwenye mkutano huo  wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna wa Polisi Janeth Magomi akiyaomba mashirika kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuimarisha usalama.\

Mwenyekiti wa kamati ya amani na maridhiano Mkoa wa shinyanga Shekh Balilusa Khamis akiwasihi kuzingatia maadili na kushirikiana pamoja katika kutokomeza vitendo vya ukatili.

Mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.Mwenyekiti wa taasisi ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga  leo Jumatano Julai 5,2023.

Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga  leo Jumatano Julai 5,2023.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: