Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas ametoa zawadi ya nafaka  na vitoweo mbalimbali baada ya kufurahishwa na kazi zinazofanywa na viongozi wa Wilaya na Mkoa wa Shinyanga  ikiwemo kamati ya siasa pamoja na kamati ya ulinza na usalama.

Mhe. Paschal Patrobas Katambi ameipongeza kamati ya siasa kupitia chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga  kwa kuendelea kutekeleza vyema majukumu yao wakishirikiana na kamati ya ulinzi na usalama katika kuimarisha amani Wilaya na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla.

Ametoa zawadi ya Ng’ombe wawili (2), kuku kumi (10) pamoja na kilo 200 za mchele huku akikemea suala la ukatili unaoendelea kufanyika kwenye jamii katika Mkoa wa Shinyanga.

Amesema Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa Mikoa yenye amani na utulivu katika masuala ya kisiasa ambapo amewaoma kuendelea kuimarisha usalama huo ili kuepukana na migogoro ambayo hurudisha nyuma maendeleo.

Mhe. Katambi pia amezipongeza kamati hizo kwa usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo amesema hatua hiyo inachochea kuongezeka kwa mapato ya ndani katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika shughuli za utekelezaji wa ilani ya CCM ikiwa lengo ni kuongeza uchumi kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amemshukuru na kumpongeza Mhe. Katambi kwa uthubutu wake katika kuchochea maendeleo Mkoani Shinyanga.

Aidha RC Mndeme amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuleta fedha zaidi ya Bilioni Mia saba kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo amewahakikishia wananchi kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyokusudiwa na serikali katika kuleta matokeo chanya Mkoani Shinyanga.

Amesema serikali ya Mkoa wa Shinyanga itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu watakao bainika kuvuruga amani  kwa kufanya uhalifu ikiwemo vitendo vya ukatili huku akiwataka wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kufuata sheria, kanuni na taratibu za Nchi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema chama hicho kitaendelea kumuunga mkono Mhe. Katambi katika shughuli zake za maendeleo za kiserikali na chama huku akimpongeza na kumshukuru kwa zawadi hizo.

Hafla ya kukabidhi zawadi ya nafaka na vitoeo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Gasper Kileo.

Zoezi la kukabidhi zawadi ya nafaka na vitoeo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas kwa kamati ya siasa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya na mkoa wa  Shinyanga likiendelea leo Jumanne Julai 25,2023.

Zoezi la kukabidhi zawadi ya nafaka na vitoeo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas kwa kamati ya siasa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya na mkoa wa  Shinyanga likiendelea leo Jumanne Julai 25,2023.

Kilo 200 za mchele pamoja na kuku kumi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas wa kwanza upande wa kulia, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa wa pili kutoka upande wa kulia akimpongeza Mhe. Katambi kwa zawadi hizo.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: