JWT YAJIPANGA KUPAZA SAUTI ILI KUWATETEA NA KUKEMEA KERO ZA WAFANYABIASHARA.


Na Mwandishi Wetu, Tanga.


Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania (JWT), imejipanga Kuhakikisha inapaza sauti Katika Kuhakikisha inatetea na kukemea kero za wafanyabiashara pamoja na kupokea maoni na Mapendekezo yao nchini na kuzifikisha sehemu husika.


Hayo yameyasema leo julai 25,2023 na Mwenyekiti wa wafanyabiashara Tanzania Hamis Livembe katika mkutano na wafanyabiashara mkoani Tanga.


Amesema wafanyabiashara hao wanapaswa kuungana na Kuhakikisha wanakuwa na sauti ya pamoja katika kuhakikisha wanajenga jumuiya yao kwa kutetea masilahi ya biashara zao.


Livembe amesema umoja wa wafanyabiashara unasaidia katika kutoa kero na kuisaidia serikali katika kutatua changamoto za wafanyabiashara pamoja na kuundwa kwa sera bora ya kibiashara



" Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ipo Katika kusaidia na kutatua kero za wafanyabiashara kwa makundi sio kwa mtu mmoja mmoja ndo maana waliunda kamati maalum ambayo lengo lake lilikuwa ni kukusanya na kuchakata na kuwasilisha kwa serikali" Amesema Livembe.


Kwa upande wake katibu wa Mkoa wa Tanga Ismail Masod amesema mpaka sasa bei ya vitenge imeshuka ikilinganishwa na hapo awali ilivyokuwa shillingi milioni 200 hadi milioni 300 ila sasa ni milioni 60 kwa kontena hizo zikiwa juhudi za kamati iliyoundwa.


Pia amewataka wafanyabiashara wa Tanga kutumia fursa ambazo serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka na waaze kuagiza mizigo china kutokana na mfumo mzuri ambao serikali imeutengeneza.


Naye Mwenyekiti wa kariakoo Martin Mbwana amesema kuwa serikali ipo pamoja na jumuiya hiyo hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kutambua fursa na thamani ambayo Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo ameitoa kwa wafanyabiashara hao.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: