Na Mapuli Misalaba, ShinyangaMkoa wa Shinyanga umeungana na Mikoa mingine Nchini kuadhimisha siku ya Mashujaa kitaifa ambapo  serikali imesema kwa kutambua na kuthamini  mchango wao, itaendelea  kuwakumbuka na kuwaenzi Mashujaa wote wa Tanzania walipoteza maisha wakati wakipigania  Taifa lao

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliyofanyika Mjini Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesema ni wajibu wa kila mtanzania kuwakumbuka mashujaa wote ambao walijitoa mhanga kupambana dhidi ya ukoloni kwa ajili ya maslahi ya Taifa

Amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa mashujaa hao serikali iliweka siku maalumu ya kuwakumbuka mashujaa hao kama ishara ya kuwaenzi

Afisa Mteule Daraja la Pili Thomas Nyabitwano ni Askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambaye ni mmoja wa mashujaa waliopigana vita vya kagera dhidi ya Uganda mnamo Mwaka 1978.

Amewaomba askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu huku wakitanguliza mbele uzalendo  kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Watemi Mkoa wa Shinyanga Chief Kidola Njange ameomba watanzania hasa vijana kuendelea kuilinda na kuidumisha amani ya Tanzania.

Julai 25, ya kila Mwaka watanzania huadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mashujaa wa Tanzania.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yakiendelea katika mnara wa mashujaa  Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: