Na John Walter-Manyara

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amewaomba wana CCM  kutambua kuwa miradi yote ya maendeleo inayoonekana katika maeneo yao ni maelekezo, maagizo na ahadi zinazotokana na Chama hicho.

Amesema sifa zote ambazo zinatokana na utekelezaji wa mema hayo lazima zihusishwe na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Chama Cha Mapinduzi ambacho yeye ndiye Mwenyekiti wake.

Akizungumza leo Julai 24, 2023 mjini Babati wakati wa kikao cha ndani cha Chama Mkoa wa Manyara, Kinana ametumia nafasi hiyo kusisitiza sifa ni lazima ziende kwa Chama cha Mapinduzi   kwa sababu ndio kinayokwenda mbele ya wananchi kuomba kura.

“Tukijenga shule inatokana na Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa na sera nzuri pamoja na  ahadi zinazotekelezeka, kwa hiyo mafanikio lazima yahusishwe na Ilani na sera za Chama Cha Mapinduzi.

“Msisahau Chama Cha Mapinduzi kinaongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali inaongozwa na Rais Samia, kwa hiyo ni mafanikio ya Chama chini ya uongozi wa Rais Samia, ni vema katika mafanikio hayo mkamtaja Rais, lakini msisahau kuitaja CCM,” amesema Kinana.


Share To:

Post A Comment: