Na John Walter-Babati

Wafanyakazi wa Kampuni ya Mati super Brands Ltd wamejitokeza kuchangia Damu katika benki ya damu salama katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara.

Jumla ya Chupa 48 za damu zimepatikana.

Kampeni hiyo ya changia damu okoa maisha,imeanzishwa na Msanii maarufu wa vichekesho nchini Rosemary Urio maarufu kama Katarina wa Karatu ambayo ilianza mwaka 2020 na Hadi sasa ameshasaidia damu mara 12, moja mkoani Manyara, mara 11 mkoa wa Arusha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo leo Julai 15,2023, Katarina amewataka wasanii na watu maarufu wajitolee kutoa damu na kuhamasisha wengine.

Amesema anafanya hayo kwa Upendo  lengo lengo likiwa ni Kusaidia wahanga wa ajali, kina Mama wanaojifungua na wote wenye uhitaji wa damu.

Meneja masoko na manunuzi wa Kampuni ya Mati super Brands Ltd Gwandume Mpoma amesema ni utaratibu walionao  kujitoa kusaidia mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo kuchangia damu.

Katibu wa Afya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara Vailine Osward  amempongeza Katarina na Kampuni ya Mati super Brands Ltd kwa uamuzi huo wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wengine.
Anna Fissoo mtumishi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara amesema aliona umuhimu wa kuchangia damu baada ya kupungukiwa wakati akijifungua.

James Misanga mratibu wa huduma za damu Salama mkoa wa Manyara, amesema damu ni uhai hivyo kila mmoja ni muhimu kuchangia kwa sababu huwezi jua ni wakati gani itakusaidia.

Mtu anayepaswa  kuchangia damu awe na umri iaka 18 na kuendelea,uzito usiopungua kilo 50, asiwe na maradhi kama shinikizo la damu au kisukari,  mjamzito au mwanamke anayenyonyesha. 

Dr James amesema muda wa kuchangia damu ni Miezi minne kwa Mwanaume na mwanamke kila baada ya miezi mitatu.
Kila robo mwaka Kuna zoezi la uchangiaji damu Kitaifa.

Ikumbukwe kwamba Wachangiaji wenye kadi wanaweza kupewa damu wanapokuwa na uhitaji.
Share To:

Post A Comment: